STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 2, 2013

Stephano Mwasyika atua Ruvu Shooting

http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2012/03/Stephano-Mwasika.jpg
Stephano Mwasyika
 WAKATI dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa rasmi leo, klabu ya soka ya Ruvu Shooting imekamilisha usajili wake kwa kuwanyakua nyota wa zamani wa Yanga na African Lyon na kukamilisha idadi ya wachezaji saba wapya iliyowanyakua kwa msimu ujao.
Afisa Habari wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Masau Bwire aliwataja wachezaji waliokamilisha usajili wao ni beki wa kushoto, Stephano Mwasyika aliyekuwa Yanga na kipa Abdul Juma Seif aliyekuwa akiidakia Lyon kabla ya kushuka daraja msimu uliopita.
Bwire alisema wachezaji hao wanaoungana na Juma Seif 'Kijiko' (Yanga), Cosmas Ader (Azam), Elias Maguli (Prisons-Mbeya), Juma Nade (Kagera Sugar) na Jerome Lembeli (Ashanti United) ambao walisajiliwa awali dirisha la usajili lilipofunguliwa mara baada ya kumalizika kwa ligi.
Wachezaji hao saba wapya wanachukua nafasi ya wachezaji watano waliotemwa katika kikosi hicho ambao ni Paul Ndauka,  Charles Nobert, Gido Chawala, Frank Mabande na Liberatus  Manyasi.
Bwire alisema wachezaji wote wa timu yao kwa sas wapo kambini pamoja na makocha wao kwa ajili ya kujiandaa na pambano lao la ufunguzi wa Ligi Kuu inayoanza Agosti 24 dhidi ya timu ya Prisons Mbeya.
Aliongeza kuwa katika kujiweka sawa kesho jioni kikosi chao kinatarajiwa kushuka dimba la Mabatini, Mlandizi Pwani kuvaana na Mabingwa wa soka mkoani humo, Kiluvya United katika pambano la kirafiki.
Bwire alisema mchezo huo ni muendelezo wa programu za benchi lao la ufundi chini ya kocha Charles Boniface kupima vijana wao kabla ya kuanza kwa ligi hiyo msimu wa 2013-2014.

No comments:

Post a Comment