STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 23, 2014

MAUAJI YA KIKATILI DAR USTAADH AMCHINJA MTOTO


* Muuaji naye auawa, kumbe mgonjwa wa akili
* Alijaza damu kwenye ndoo
Add caption

mwili wa maremu mtoto Jamali aliechinjwa na ustadhi mbagala charambe mianzini
mwili wa marehem ustadhi mohamed kurangwa aliemchnja mtotoukishushjwa katika hospitali ya Temeke
baadhi ya wakazi wakichungulia nyumba lililotokea tukio la mauaji ya kikatili







USTAADH Mohamed Kurangwa (36), aliyemuua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nzasa Jamal Salum (12)  kisha naye kuuawa, ametajwa kuwa alikuwa ana matatizo ya akili.
Kurangwa alimuua Jamal mwanafunzi wa darasa la tano juzi jioni nyumbani kwake Mbagala Charambe Mianzini,  kwa kumchinja na kuweka kichwa cha marehemu huyu kwenye miguu ya mtoto huyo, kisha kuupeleka mwili wake choo cha nyumba anayoishi, muuaji.
Muuaji huyo alizoa  damu ya Jamal na  kuijaza kwenye ndoo kisha  kuiweka pembeni ya nyumba yake kabla ya kuingia chumbani kwake, kujifungia na kusoma Koran.
Ustaadhi Kurangwa  ambaye  aliuawa na wananchi,  wakati wa uhai wake alikuwa Imam wa msikiti wa Kareem ulioko Charambe.
MATATIZO YA AKILI
Mdogo wa muuaji  Daudi Kurangwa alisema  kati ya mwaka 1996-1997 marehemu kaka yake alishawahi kuugua ugonjwa wa akili na kutibiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Alieleza kuwa baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali alikuwa akiendelea kutumia dawa kwa kipindi  lakini aliziacha baada ya kuhisi amepona.
“Kati ya Juni na Julai mwaka jana aliugua tena  na kutibiwa katika hospitali ya Temeke,” alisema na kuongeza kuwa hata hivyo juzi Kurangwa hakuwa na dalili zozote za ugonjwa huo kumrudia.
Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Polisi Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia tatizo la akili ,  alisema polisi inaendelea na uchunguzi na kueleza kuwa kuna taarifa kuwa muuaji kipindi cha nyuma aliwahi kuugua maradhi ya akili na kwamba kwa hivi karibuni alikuwa ni mzima na hajawahi kuonekana kama anaumwa.
Kamanda Shana alisema ukweli wa tukio hilo haujafahamika na kwamba Kanda Maalum ya Dar es Salaam imeunda kikosi kazi cha kuchunguza tukio hilo.
USHUHUDA WA RAFIKI
Akizungumza na NIPASHE Jumapili nyumbani kwa wazazi wa marehemu Jamal, rafiki wa mtoto huyo aliyenusurika kifo,  Ramadhani Hamisi (11) anayesoma darasa la tano katika  Shule ya Msingi Chemchem, alisema kabla ya kuchinjwa Ustaadhi Kurangwa alianza kumchoma visu mfululizo shingoni..
Ramadhani alisema anaishi na mjomba wake katika nyumba ya Ustadh huyo iliyoko Mianzini Njiapanda, sehemu ambapo imamu huyo alimchinja Jamal
“Siku  ya tukio nilimuomba marehemu Jamal, anisindikize kwenda nyumba  kuchukua kalamu, ilikuwa  saa 10:30 baada ya kupata kalamu hiyo ndani ya chumba tunachoishi na mjomba tulifunga mlango na kuanza kuondoka.
“Wakati  nafunga mlango marehemu Jamal alikuwa jirani yangu akiwa ameshika  madaftari na kalamu,” alisema Ramadhani kwa uchungu.
Aliendelea kueleza kuwa mara Ustadh Kurangwa alitokea akiwa na baiskeli, alipowaona aliiweka pembeni na kuja karibu nao akafungua pazia la mlango wa chumba chake, lakini wakati wanataka kuondoka, ghafla alimkamata Jamal na kuanza kumchoma  kisu sehemu mbalimbali shingoni.
"Nilimshuhudia akimchoma kisu  mara nyingi, Jamal alilia  akisema nisamehe Ustadh, nisamehe Ustadh," aliongeza mtoto huyo huku akitokwa na machozi.
Ramadhani alikimbia hadi nyumbani kwa Jamal  na kumueleza mama yake kuhusu tukio hilo na yaliyoendelea nyuma hakuweza kuyashuhudia tena.
JAMAL ACHINJWA
Mjumbe wa nyumba kumi wa Mtaa wa Mianzin,  Ester Msumba, aliyesema alikuwa wa kwanza kushuhudia tukio hilo, alieleza kuwa  alifika eneo la mauaji baada ya kumsikia  mwanamke mmoja akipiga mayowe kuomba msaada baada ya kuona kiwiliwili cha mtoto kimelala na kichwa chake kimewekwa miguuni.
Alisema mwanamke huyo alikwenda kwenye madrasa ya Ali Munawar  kumpeleka mtoto wake kwa ajili ya kumuanzishia masomo ya ziada, kwa vile licha ya kufundisha dini eneo hilo alilokuwa anaishi Kurangwa linatoa mafunzo hayo ya ziada.
"Baada ya kusikia sauti ya yule mama  nilikimbilia eneo la tukio, hapo nilikuta hali ni mbaya kwani niliona  mwili wa mtoto umelazwa chooni na kichwa chake kiliwekwa miguuni kwake," alisema msumba.
Alisema wakati wa mauaji hayo sauti ya mtoto Jamal  haikusikika hivyo ilikuwa vigumu kupata msaada.
Msumba alisema pamoja na mwili huo, alishuhudia ndoo iliyokuwa na damu iliyochanganywa na maji  kitu kilichoashiria muuaji alikinga damu hiyo kuzuia isitapakae na kusambaa chini.
Sakafu ya choo hicho ilikuwa imejaa damu na familia ilizuiliwa kukitumia kwa muda kupisha uchunguzi.
Baada ya kufanya tukio hilo, Ustadh Kurangwa, alikwenda chumbani kwake na kujifungia huku akisoma Kuran.
"Baada ya kumtafuta kwa muda mtu aliyefanya unyama huo, tuligundua   amejifungia ndani tulipomchungulia tulimuona akisoma Kuran huku kanzu yake ikiwa imetapakaa damu," alisema mjumbe huyo.
USTADHI KURANGWA AUAWA
Wananchi walimvamia  chumbani baada ya kubomoa dirisha na  kumshambulia kwa matofali na mawe hadi alipopoteza fahamu na kumvua nguo kisha kumtoa nje na  kumpiga  hadi alipokata roho.
WAZAZI WA JAMAL
Habiba Selemani (27) mama mzazi wa marehemu Jamal akizungumza na gazeti hili alisema anamuachia Mungu  kifo cha mwanawe.
"Namuachia Mungu kwanini  tukio hili afanyiwe Jamal," alisema mama mzazi, hata  hivyo, alikumbukia kuwa  kabla ya kifo chake  alikuwa anacheza na mdogo wake mwenye miezi sita na kumvisha nguo  alipomaliza aliniaga kwamba anakwenda kucheza.
"Aliniambia anakwenda kucheza lakini kwa mshangao alinieleza kuwa anaona nyota nyingi, sikujali nilimuacha aende zake," aliongeza kusema.
Kwa upande wake   Salimu Ally, ambaye ni baba mzazi, alisema amepokea msiba huo  mshituko mkubwa na hakuamini kilichotokea kwani ni  tukio  la kinyama.
Alieleza kuwa juzi  jioni wakati anakaribia  nyumbani aliwaona wanawake  wanaingia kwenye  nyumba hiyo yalikofanyika mauaji ya  mwanae na kushangaa kwani walikuwa  wanatoka na kulia.
Ally alisema hakujua kilichotokea na kwamba mawazo yake yalikuwa kufika nyumbani kwanza.
“Nilipofika nilimkuta mke wangu analia hajitambui ndipo mpangaji mwenzangu aliponieleza kuwa  mwanangu Jamal  kachinjwa niliumia sana , sikuweza kuamini,” alisema kwa huzuni.
Alikanusha kuwa marehemu mtoto wake alikuwa anasoma kwenye chuo cha Ustaadh huyo na pia hawafahamiani  japo Kurangwa  alimwita na kuingia naye ndani kisha kumchinja.
Mwili wake ungezikwa jana saa 10 jioni  baada ya kupatiwa kibali cha polisi kuchukua maiti kutoka hospitali ya Temeke.
Chanzo:NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment