STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 23, 2014

PSG yaifumua Toulouse nyumbani, Ibrahimovic apiga hat-trick

Zlatan Ibrahimovic akishangilia moja ya mabao yake wakati wakiiangamiza Toulouse nyumbani kwao.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Ufaransa, PSG imeendelea kuonyesha dhamira yao ya kutetea taji hilo baada ya kupata ushindi wa kishindo ugenini dhidi ya Toulouse walipoilaza mabao 4-2, huku Zlatan Ibrahimovic akifunga hat-trick yake tatu msimu huu katika ligi hiyo.
Ibrahimovic alianza kwa kufungwa kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 32 kabla ya Wissam Ben Yedder kusawazisha dakika moja kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili wageni waliingia kivingine kwa kulisakama lango la wenyeji wao na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Ezequeil Lavezzi katika dakika ya 56 kabla ya Ibarhimovic kurejea tena nyavuni kwa kufunga bao la tatu dakika ya 68 akimalizia kazi nzuri ya Yohan Cabaye.
Ben Yedder alifunga bao la pili kwa wenyeji katika dakika ya 72 na dakika moja kabla ya mchezo huo kumalizika nyota wa Sweden, Ibrahimovic alikamilisha hat-trick yake kwa kufunga bao la nne lilil;oifanya PSG kujikita zaidi kileleni ikifikisha pointi 61 baada ya michezo 26.
Katika mechi nyingine Rennes ilipata ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nantes kwa mabao ya Ntep, Konradsen na Toivonen.

No comments:

Post a Comment