STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 23, 2014

Simba yafa Taifa, Azam yashindwa kurudi kileleni

 * Yabanwa na Prisons wakiruhusu bao jioni
Simba iliyokufa Taifa mbele ya maafande wa JKT Ruvu
Azam iliyoshindwa kurejea kileleni baada ya kulazimishwa sare ya 2-2
JKT walioitafuna Simba uwanja wa Taifa
Prisons walioendeleza maajabu yake katika duru la pili
WAKATI Azam ikishindwa kurejea kileleni baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Prisons, 'Wekundu wa Msimbazi', Simba wameendelea kugawa pointi baada ya kuangukia pua mbele ya JKT Ruvu kwa kufungwa 3-2.
Simba inayonolewa na kocha Zdrakov Logarusic 'Loga' ilijikuta ikipoteza pointi 10 katika mechi ya nne baada ya maafande wa JKT Ruvu chini ya kocha Fred Felix Minziro kushtukiza kwa kipigo hicho leo jioni.
Mabao ya Husseni Bunu katika dakika ya 13 na Emmanuel Switta dakika ya 44 na 53 yalitosha kuinyong'onyesha Simba iliyokuwa inarejea nyumbani jijini Dar es Salaam baada ya kupata matokeo mabovu ugenini ikiambulia pointi mbili katika mechi zake tatu.
Hata hivyo vijana wa Simba walipambana na wapinzani wao waliokuwa pungufu na kufanikiwa kurejesha mabao mawili yalifungwa kwa mikwaju ya penati na Amissi Tambwe moja likiwa la penati dk 74 na 86.
Kwa kipigo hicho Simba imesalia kwenye nafasi ya nne ya msimamo ikiwa na pointi zake 32, tatu pungufu na Mbeya City ambayo nayo jana ililala mbele ya Coastal Union ya Tanga kwenye mfululizo wa ligi hiyo.
Katika mechi nyingine iliyochezwa uwanja wa Chamazi, Prisons Mbeya imeendelea kujikongoja baada ya kuibana Azam na kulazimisha sare ya mabao 2-2.
Bao la kusawazisha la Prisons lilifungwa zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mchezo huo kuisha wakati Azam wakiamini wameibuka na ushindi na pengine kurejea kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya jana kushushwa na Yanga iliyoifumua Ruvu Shooting kwa mabao 7-0.
Wageni Prisons ambao wanafikisha mechi ya tano bila kupoteza mchezo wowote ikijikusanyia jumla ya pointi 11 ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwana na Omega Seme kabla ya Aggrey Morris kuisawazisha.
Kipre Tchetche aliiongozea Azam bao la pili ilikiwa bao lake la 10 kabla ya kuja kutolewa kwa kadi nyekundu kutokana na kupewa kadi ya njano ya pili.
Laurian Mpalila aliiokoa Prisons isiadhirike baada ya kufunga bao la pili na la kusawazisha zikiwa zimeshalia dakika  mbili kabla ya kumalizika kwa pambano hilo na kufanya timu hizo zigawane pointi moja moja.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014    
                                  P    W     D    L    F     A   GD  PTS

01.Yanga                   17   11    05   01   41   12   29  38
02.Azam                    17   10    07   00   31   12   19  37
03.Mbeya City           19   09    08   02   24   16   08  35
04.Simba                    19   08    08   03   35   19   16  32
05.Kagera Sugar         19   06    08   05   16  15   01  26
06.Coastal Union        19   05    10    04  14  09   05  25
07.Mtibwa Sugar        19   06    07    06   23  23   00  25
08.Ruvu Shooting        19  06    07   06    20  26  -06  25
09.JKT Ruvu              19   07    01    11   16  29  -13  22
10.Prisons                   18   04    08    05   17  18  -01  20
11.Mgambo                19   05    05    09   12  27  -15  20
12.Oljoro                    20   02    09    09   15  30  -15  15
13.Ashanti                   18   03    05    10   15  30  -15  14
14.Rhino Rangers        19   02    07    10   12  23  -11  13

Wafungaji:
17- Tambwe Amisi (Simba)
10- Kipre Tchetche (Azam)
09- Elias Maguri (Ruvu Shooting) Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu (Yanga)
08-Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Mrisho Ngassa (Yanga)
07- Peter Michael (Prisons)
06- Themi Felix (Kagera Sugar), Mwegani Yeya (Mbeya City)
05- Tumba Sued (Ashanti Utd), Jerry Santo (Coastal Union)
04- Jerry Tegete (Yanga), Jonas Mkude, Betram Mombeki (Simba), Bakar Kondo, Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerome Lambele (Ruvu Shooting), Abdallah Juma (Mtibwa Sugar)
03- Haruna Chanongo, Ramadhani Singano (Simba), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu) Humphrey Mieno, Mcha Khamis (Azam), Amir Omary (Oljoro), Jeremia John (Mbeya City), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Simon Msuva (Yanga), Emmanuel Switta(JKT Ruvu), Laurian Mpalila (Prisons)

No comments:

Post a Comment