STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 23, 2014

Liverpool, Newcastle Utd zashinda England

Jordan Henderson
Jordan Henderson akifunga moja ya mabao yake
Newcastle striker Loic Remy shoots past keeper Brad Guzan for his side's winner against Aston Villa
Luic Remy akifunga bao dakika za jioni likiizima Aston Villa
LIVERPOOL imeendelea kujiimarisha kwenye nafasi ya nne baada ya jioni hii kuikwanyua Swansea City kwa mabao 4-3, huku Newcastle United ikipata ushindi nyumbani dhidi ya Aston Villa kwa bao 1-0 katika Ligi Kuu ya England.
Mabao mawili ya Daniel Sturridge na mengine kama hayo ya Jordan Henderson yalitosha kuizima Swansea iliyokuwa ugenini kwa kuisaidia Liverpool kufikisha jumla ya pointi 56 na kuendelea kujikita kwenye nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo.
Sturridge aliiandikia bao Liverpool dakika ya tatu tu ya mchezo akimalizia kazi nzuri ya Raheem Sterling, kabla ya Henderson kuongeza la pili dakika ya 20 kwa pasi ya Sturridge kabla ya Jonjo Shelvey dakika tatu baadaye  na wageni kusawazisha bao dakika ya 26 kupitia kwa Winfried Bony na Sturridge kufunga bao la tatu dakika ya 36 kwa pasi ya Luis Suárez.
Kipindi cha pili kilianza kwa Bony kufunga bao la kusawazisha dakika mbili baada ya mapumziko kwa mkwaju wa penati na Henderson alifunga bao la ushindi dakika ya 74.
Katika mechi nyingine, Newcastle United ikiwa nyumbani iliitandika Aston Villa kwa bao 1-0 , goli hil;o likiwekwa kimiani na  Luic Remy dakika za nyongeza kabla ya pambano hilo kumalizika.
Kwa ushindi huo Newcastle United imechupa hadi nafasi ya nane ikifikisha pointi 40 huku Aston Villa ikisaliwa na pointi zake 28 ikishika nafasi ya 13.

No comments:

Post a Comment