STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 13, 2014

Twanga Pepeta kuinogesha Valentine Day kesho Mzalendo Pub


BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ wanatarajia kuwapagawisha wapendanao watakapofanya onyesho maalum siku ya ‘Valentine Day’, kesho Ijumaa.
Onyesho hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, litajulikana kama 'Dodoma Wine Valentine Show'.
Mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga amesema onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Dodoma Wine, Freditto Entertainment na Saluti5.
Kapinga alisema siku hiyo Twanga Pepeta watatambulisha nyimbo na staili mpya ya uchezaji.
Mratibu huyo alisema kuwa siku hiyo Twanga Pepeta pia itapiga nyimbo zao za zamani zilizowapatia umaarufu.
Baadhi ya nyimbo hizo ni Kisa Cha Mpemba, Fainali Uzeeni, Mtu Pesa, Safari 2005, Aminata, Busu  2000 na nyinginezo.
Bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigono pia itapiga nyimbo zao za kisasa kama 'Nyumbani ni Nyumbani', 'Dunia Daraja',  ‘Mwana Dar es Salaam’, ‘Shida ni Darasa’, ‘Rafiki Adui’, ‘Mwisho wa Ubaya ni Aibu’, ‘Nazi Haivunji Jiwe’ na ‘Sitaki Tena’.
Bendi hiyo inaundwa na wanamuziki kama Kalala Junior, Dogo Rama, Saleh Kupaza, Luiza Mbutu, Badi Bakule, Greyson Semsekwa, Rama Pentagon, Mirinda Nyeusi, Kala Junior, na Janet Isinika katika safu ya uimbaji.
Kwa upande wa upigaji vyombo wapo James  Kibosho, Jojo Jumanne, Moshi Kinanda, Miraji Shakashia, Gody Kanuti, Kaposho, huku safu ya unenguaji ikiwa, Saidi Matongee, Mandela, Abdilah Zungu,  Sabrina Pazi, Vicky, Hamida na Grace.

No comments:

Post a Comment