STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 13, 2014

Messi aipeleka Barca fainali ya Mfalme akiweka rekodi ya mabao


MABINGWA  watetezi wa Ligi Kuu ya Hispania usiku wa kuamkia leo imetinga Fainali ya Kombe la Mfalme wakiifuata Real Madrid, huku mshambuliaji wake Lionel Messi akiweka rekodi ya kufunga mabao mengi kwa klabu hiyo.
Messi alifunga bao la kuongoza katika mchezo huo dakika ya 27 na kuipa sare ya 1-1 timu yake dhidi ya Real Sociedad na kufikisha mabao 335 hivyo kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika klabu hiyo ya Hispania.
Wenyeji walisawazisha bao hilo dakika tatu kabla ya mechi hiyo ya marudiano baina ya timu hizo kupitia kwa Griezmann na kuivusha Barca kwa jumla ya mabao 3-1 kwani katika mechi ya awali Real walifungwa ugenini mabao 2-0 na Barcelona.

No comments:

Post a Comment