STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 13, 2014

Twiga Stars yatua salama yaahidi mapambano

Twiga Stars
KIKOSI cha wachezaji 19 wa Twiga Stars kimetua salama mjini Lukasa, Zambia (Februari 13 mwaka huu) huku Kocha Mkuu Rogasian akiahidi ushindani kwenye mechi dhidi ya wenyeji itakayochezwa Uwanja wa Nkoloma.

Kocha Kaijage aliwaambia waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda mara baada ya kikosi chake kutua kwa ndege ya Fastjet saa 3.30 asubuhi kwa saa za Zambia kuwa wamekuja kushindana, na si kushiriki.

Twiga Stars ambayo mara ya mwisho ilikutana na Zambia kwenye michuano ya COSAFA miaka miwili iliyopita na kuibuka na ushindi imefikia hoteli ya
Golden Peacock, na katika uwanja wa ndege ilipokewa na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zambia (FAZ) na Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, Jeswald Majuva.

Timu hiyo leo saa 9 alasiri kwa saa za Zambia ambapo Tanzania ni saa 10 jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nkoloma ambao ndiyo utakaotumika
kwa mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayochezwa kesho.

Wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwapewa Mtumwa, Sherida Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.

RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kesho
(Februari 14 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waaandishi wa habari za
michezo.

Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo
ghorofa ya tatu katika jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden na Ohio jijini
Dar es Salaam.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
+260 976375482
Lusaka, Zambia

No comments:

Post a Comment