Tevez akishangilia moja ya mabao yake |
KLABU ya AC Milan imezinduka nchini Italia baada ya juzi kuikwanyua Fiorentina kwa mabao 2-0 nyumbani kwao, huku usiku wa jana wapinzani wao wa jiji la Milan, InterMilan walilazimishwa sare ya 0-0 na Udinese.
Milan ambaye imekuwa na matokea mabaya kwenye Ligi Kuu ya Seria A, walipata ushindi huo kupitia magoli yaliyofyungwa na Mexes dakika ya 23 kabla ya Mario Balotelli kufunga kipindi cha pili katika dakika ya 64 na kuipaa pointi tatu mabingwa hao wa zamani wa Ulaya.
Katika mechi nyingine za ligi hiyom, Juventus wakiwa nyumbani walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Parma na kuzidi kujiweka karibu na kutetea taji la ubingwa wa ligi hiyo.
Magoli yote mawili yalitupiwa kambani na Carlos Tevez katika dakika ya 25 na 32 na kuwapa pointi zinazowafanya wafikishe 81 na kusaliwa na mechi nane mkononi ambapo kama akishinda mechi tatu ikiwamo ya Jumapili dhidi ya Napoli atatawaza kuwa bingwa. Wageni walimpoteza Amauri aliyeonyesha kadi nyekundu.
Matokeo ya mechi nyingine za ligi hiyo;
Chievo 3 - 0 Bologna
Cagliari 1 - 0 Hellas Verona
Genoa 2 - 0 Lazio
Atalanta 2 - 0 Livorno
Fiorentina 0 - 2 Milan
Catania 2 - 4 Napoli
Juventus 2 - 1 Parma
Sassuolo 1 - 2 Sampdoria
Inter Milan 0-0 Udinese
No comments:
Post a Comment