SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza mchakato wa kuendeleza uwanja wake uliopo eneo la Mnyanjani jijini Tanga.
Rais
wa TFF, Jamal Emil Malinzi alisema shughuli
inayoendelea kwa sasa ni kupima udongo (soil test) na kuandaa michoro
kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha michezo (Sports Complex) ukiwemo uwanja
wa mpira wa miguu na majukwaa yake.
Amesema
TFF imetuma maombi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuomba eneo la
kujenga kituo cha michezo ikiwemo uwanja wa mipira wa miguu na majukwaa
yake.
“Pia
Mkuu wa mkoa ameombwa kuingilia kati kuwaondoa wafanyabiashara
waliovamia uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri (King George Memorial
ground) mjini Moshi,”amesema Malinzi.
Amesema
TFF inawakumbusha viongozi wa vyama vya mikoa ambao hawajaomba maeneo
ya kujenga vituo vya michezo vikiwemo viwanja vya mpira wa miguu,
waongeze jitihada za kufanya hivyo na shirikisho hilo litawaunga mkono.
“TFF
inachukua fursa hii kuvipongeza vyama vya mpira wa miguu ambavyo ama
tayari vimeshachukua hatua au viko mbioni kuchukua hatua kutafuta na
kuendeleza maeneo kwa ajili ya matumizi ya mpira wa miguu. TFF inaahidi
kuunga mkono juhudi hizi na pale itakapohitajika kuongeza nguvu
haitasita kufanya hivyo,”amesema.
No comments:
Post a Comment