STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 24, 2014

Arsenal yaingia mbio za kumwinda van Gaal

http://www.101greatgoals.com/wp-content/uploads/2014/04/Louis-Van-Gaal-Bayern-Mun-001.jpg
Kocha van Gaal
 KLABU ya Arsenal imedaiwa kufanya mawasiliano na kocha Louis van Gaal, anayetajwa kuchukua mikoba ya David Moyes aliyetimuliwa na klabu ya Manchester United juzi.
Duru za kispoti zinasema kuwa, Arsenal imelazimika kuwasiliana na Mholanzi huyo kutokana na kutokuwa na uhakika na mustakabaliwa wa kocha wake Arsene Wenger. 
Hata hivyo Arsenal bado ina matumaini kuwa Wenger atasaini mkataba mpya wa miaka miwili waliokubaliana Octoba mwaka jana, lakini inajulikana anaweza kujiuzulu kama akishindwa kufikia malengo aliyojiwekea baada ya kumalizika kwa msimu. 
Imebainika kuwa Mfaransa huyo aliwaambia marafiki zake kuwa anafikiria kuacha kuinoa Arsenal kama awatashinda Kombe la FA na kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu. 
Kutokana na hali hiyo kumekuwa na mipango ya muda mfupi inayofanywa na Arsenal, mojawapo ni kujaribu kufanya mazungumzo na Van Gaal ambaye mkataba wake na timu ya taifa ya Uholanzi unamalizika baada ya Kombe la Dunia.
Mbali na kuwindwa na Arsenal, kocha huyo pia amekuwa akitajwa kunyemelewa na klabu za Manchester United na Tottenham Hotspurs ambao nao wanataka achukue nafasi ya Tim Sherwood mwishoni mwa msimu huu.
Kocha huyo mwente rekodi za kuvutia amekuwa akiwania kutokana na uwezo wake wa kuwaongoza na kuwadhibiti wachezaji hata wale wakorofi. 

No comments:

Post a Comment