STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 24, 2014

Sturridge arejea,, Chelsea ikipanga kupumzisha nyota wake

http://www3.pictures.zimbio.com/gi/Daniel+Sturridge+Liverpool+v+Fulham+Premier+HI6EojIbLKll.jpg
Daniel Sturridge
http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/03/06/article-2288964-09591184000005DC-339_306x423.jpg
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
 WAKATI kocha Jose Mourinho akidaiwa kutaka kuwapumzisha wachezaji wake nyota wake katika pambano lao la Ligi Kuu dhidi ya Chelsea ili kuitafutia kasi Atletico Madrid katika mechi ya nusu fainali ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wapinzani wao Liverpool wanachekelea kurejea kwa Daniel Sturridge.
Sturridge anategemewa kurejea kutoka katika majeruhi katika mchezo huo wa Jumapili ambao watakwaana na Chelsea.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye miaka 24 alikuwa akilalamika maumivu ya msuli katika ushindi wa mabao 3-2 waliopata dhidi ya Manchester City Aprili 13 hivyo kupelekea kutolewa nje. 
Toka apate majeruhi hayo alikosa mechi moja lakini sasa anategemewa kurejea tena uwanjani kuisaidia Liverpool katika mchezo huo muhimu ambao kama wakishinda utawafanya kuendelea kujikita kileleni hivyo kuweka hai matumaini yao ya ubingwa wa Ligi Kuu. 
Sturridge amesema kwa sasa anajisikia vyema na ni mategemeo yake atakuwepo katika mchezo huo wa Jumapili lakini itategemea kama kocha Brendan Rodgers atamchagua.
Katika hatua nyingine, Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amesema anataka kuwapumzisha nyota wake kwa ajili ya safari kwenda Anfield kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool Jumapili ijayo. 
Chelsea bado wako katika kinyang’anyiro cha taji la ligi wakiwa wamebakiwa na michezo mitatu lakini Mourinho anataka kuhamishia nguvu zake katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid. 
Katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa juzi, Chelsea iling'ang'aniwa na wenyeji wao Atletico kwa kutoka suluhu.
Hata hivyo, kocha huyo amesema uamuzi huyo wa kuwapumzisha baadhi ya nyota wake unaweza usiwe wa kwake kuufanya kwa sababu anataka kusikiliza na mawazo ya wengine. 
Kipigo cha mabao 2-1 walichopata Chelsea kutoka kwa Sunderland mwishoni mwa wiki iliyopita kinamaanisha hata kama wakishinda mchezo wa Anfield inaweza isitoshe kuizuia Liverpool kushinda taji la ligi baada ya kupita miaka 24.
Liverpool inaoongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 80, huku wapinzani wao waliopo nafasi ya pili wana pointi 75 moja zaidi ya ilizonazo Manchester City iliyo na mchezo mmoja zaidi ya timu hizo mbili za juu zilizocheza mechi 35.

No comments:

Post a Comment