STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 24, 2014

Mkenya kuzihukumu Stars na Intamba Murugamba

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbouke40Ajpgip-WYtuNcSkslDTj7_vx1cW1lSk8TTr-VrfSpd48or2vfOoU95GSaeEPAw2h5x4McRiOOgSk6nbUS6SUXQKo3lzFQl3LThJA16UJsJRVH5TDtfBRQTKxdCPu8d59WboTi_/s400/waamuzi.jpg
Mwamuzi Ogwayo atakayezichezesha Stars na Intamba Murugamba
MWAMUZI Anthony Ogwayo mwenye beji ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa keshokutwa (Aprili 26 mwaka huu)  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ogwayo katika mechi hiyo ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, atasaidiwa na Gilbert Cheruiyot na Oliver Odhiambo wote pia kutoka Kenya. Mwamuzi wa mezani atakuwa Israel Mujuni wa Tanzania.
Burundi inatarajia kuwasili nchini leo (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways na itafanya mazoezi kesho (Aprili 25 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza tangu kuanza kwa mpango wa maboresho wa timu hiyo.
Makocha wa timu zote mbili pamoja na manahodha wao kesho (Aprili 25 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mechi hiyo.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000.

No comments:

Post a Comment