STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 24, 2014

Zawadi za washindi Ligi Kuu Tanzania Bara zatangazwa

* Amissi Tambwe kuzoa Mil 5.2
* Azam kama bingwa kunyakua Mil 75
Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Azam watakaozoa Mil 75
Tambwe wa Simba kajihakikishia Sh Mil 5.2
MSHAMBULIAJI Amisi Tambwe wa Simba atalamba Sh. milioni 5.2 za zawadi ya mfungaji bora zitakazotpolewa na wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kampuni ya huduma ya simu ya Vodacom Tanzania baada ya kuibuka mfungaji bora wa msimu wa 2013/14 wa ligi hiyo.

Aidha, timu yenye nidhamu italamba Sh. milioni 16 ikiwa ni ongezekon la Sh. milioni moja ikilinganishwa na ilivyokuwa msimu uliopita.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim katika mkutano na waandishi wa habari muda mfupi uliopita kwenye ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zilizopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

ZAWADI ZA WASHINDI LIGI KUU BARA 2013/2014
Bingwa: Sh. Milioni 75
Mfungaji Bora: Sh. Milioni 5.2
Timu yenye Nidhamu; Sh. Milioni 16
Kipa Bora: Sh. Milioni 5.2
Refa Bora; Sh. milioni 5.2
  Mwalim amesema mabingwa Azam FC watazawadiwa Sh. milioni 75 ikiwa ni ongezeko la Sh. milioni 5 ikilinganishwa na ilivyokuwa msimu uliopita.   Kipa bora, mwamuzi bora watapata Sh. milioni 5.2 kila mmoja ikikwa ni ongezeko la Sh. 200,000.Timu yenye nidhamu italamba Sh. milioni 16, ikiongezeka kutoka Sh. 15 ya msimu uliopita zilizochukuliwa na Yanga.   Silas Mwakibinga, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), aliyekuwa amefuatana na Mwalim kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, alisema tarehe ya kutolewa kwa tuzo hizo itatangazwa baada ya wiki moja.

No comments:

Post a Comment