KWA HABARI ZA BURUDANI, MICHEZO NA MATUKIO MBALIMBALI
STRIKA
USILIKOSE
Tuesday, April 8, 2014
TFF yaridhia maamuzi ya Kamati ya Maadili
Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana na uamuzi uliofanywa na Kamati ya Maadili
katika malalamiko mawili ambayo iliyawasilisha mbele yake, hivyo
haitakata rufani.Katibu
Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa aliwasilisha mashauri mawili mbele ya
Kamati hiyo iliyoongozwa na William Erio. Malalamiko ya kwanza yalikuwa
dhidi ya waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA), Oden Mbaga na Samwel Mpenzu na wakufunzi wa waamuzi Riziki
Majala na Mchungaji Army Sentimea.Wote
aliwalalamikia kwa kuwafanyisha mitihani (wakufunzi), na waamuzi
kufanya mitihani hiyo kinyume na utaratibu pamoja na kughushi matokeo.Kamati
katika uamuzi wake iliiagiza waamuzi hao kufanya upya mtihani huo
katika robo inayofuata ambapo wakifaulu waendelee kuchezesha mechi.
Waamuzi wa FIFA hufanya mitihani hiyo mara nne kwa mwaka.Kwa
upande wa shauri dhidi ya Ofisa Takwimu wa TFF, Sabri Mtulla ambaye
alilalamikiwa kwa kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
kuwa hakukuwa na pingamizi dhidi ya mchezaji Emmanuel Okwi, Kamati
iliagiza suala hilo liwasilishwe upya pamoja na ushahidi wa kuthibitisha
malalamiko hayo.
No comments:
Post a Comment