STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 8, 2014

Thomas Mashali, Karama Nyilawila kuwania ubingwa wa UBO-Mabara Dar

Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika'
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJPGulwWfuBf6qU9wozguZwayMgHptdhsmYHyZc9wFEWZozMHE2d6nf9VE5hAje14ScS1QW5Vq1efAJNar_tBcC2Xielx2Lv9MQn5_9zvT9E1BXSzwW15Kj4sp5jhXYaWnpmNdubvh974/s640/DSC_1840.JPG
Karama Nyilawila 'Captain'
BINGWA wa UBO-Afrika uzito wa kati, Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' anatarajiwa kuvaana na bingwa wa zamani wa Dunia wa WBF, Karama Nyilawila 'Captain' siku ya Mei Mosi kuwania ubingwa wa Mabara wa UBO.
Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO-Limited), Yasin Abdallah 'Ustaadh' aliiambia MICHARAZO mapema leo kuwa, pambano hilo la uzito wa kati litafanyika kwenye ukumbi wa PTA Dar es Salaam.
Ustaadh alisema pambano hilo limeandaliwa na Promota Ally Mwazoa kutoka Tanga na TPBO-Limited watalisimamia kama chama wenyeji.
"Baada ya kufanikiwa kumchapa Japhet Kaseba na kutwaa ubingwa wa UBO Afrika, bondia Thomas Mashali ana nafasi nyingine ya kutwaa taji jingine atakapopanda ulingoni Mei Mosi kupigana na Karama Nyilawila," alisema.
Ustaadh alisema mabondia hao walisaini mkataba huo jana na kwamba wanaanza maandalizi kwa ajili ya mchezo huo utakaokuwa wa raundi 12 uzito wa Super Middle utakaosindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi.
Rais huyo wa TPBO-LImited, alisema anaamini ni nafasi kwa mabondia wote wawili kumaliza ubishi baina yaoe baada ya hivi karibuni Mashali kuwakejeli Nyilawila na Mada Maugo akiwafananisha na midoli na kudai hakuna wa kumweza.
Mashali aliyepigana mara 13 na kushinda michezo 10 akipigwa miwili na kutoka sare mchezo mmoja, alimtwanga Kaseba kwa pointi katika pambano lililofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita na kutwaa taji la UBO Afrika lililokuwa wazi.

No comments:

Post a Comment