STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 8, 2014

Yanga, Azam hapatoshi kesho VPL

Mabingwa watetezi Yanga watakaovaana na Kagera Sugar
Vinara wa VPL, Azam watakaoitembelea Ruvu Shooting Mabatini
Ruvu itavuna nini dimba lake la nyumbani dhidi ya  Azam kesho
Baada ya kuidindia Simba uwanja wa Kaitaba na kutoka sare ya 1-1, Kagera ya jackson Mayanja itavuna nini kwa Yanga kesho Taifa?
KIVUMBI cha Ligi Kuu ya ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 9 mwaka huu) huku timu za Azam na Yanga ambazo zipo nafasi mbili za juu zikiendelea kuchuana. Azam itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani. Nayo Yanga itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa jijini.
Joto la mechi hiyo lilianza mapema kwa Azam kuomba kuahirishiwa kutoka Jumapili hadi kesho, huku wapinzani wao wakiwasimamisha nyota wake watatu waliodaiwa kutoweka kinyemela kambini.
Wachezaji hao ambao hawatakuwepo katika mechi hiyo ya Mabatini ni Ibrahim Susan 'Chogo', Juma Seif 'Kijiko' na Cosmas Lewis. Watetezi Yanga, vinara wa ligi hiyo Azam, Ruvu Shooting na Kagera Sugar zote zimeshinda mechi zao za raundi ya 23 wakati mechi za kesho zitakuwa kwa ajili ya kukamilisha raundi ya 24 ya ligi hiyo ambayo inatarajia kukamilika Aprili 19 mwaka huu. Ligi hiyo itaingia raundi ya 25 Aprili 12 na 13 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa viwanjani. Aprili 12 mwaka huu itakuwa Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting (Manungu, Morogoro), Coastal Union vs JKT Ruvu (Mkwakwani, Tanga), na Tanzania Prisons vs Rhino Rangers (Sokoine, Mbeya).
Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo Shooting vs Kagera Sugar (Mkwakwani, Tanga), Simba vs Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mbeya City vs Azam (Sokoine, Mbeya) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
Azam inaongoza msimamo ikiwa na pointi 53 wakati Yanga wenyewe wana pointi 49 na Kagera Sugar wana 34 huku Ruvu Shooting wakiwa na 32 hali inayoonyesha upinzani ulivyo kwa timu zote nne na matokeo yoyote yanaweza kubadilisha msimamo hasa baina ya Ruvu na Kagera Sugar wanaochuana na Simba kuwania nafasi ya nne.

No comments:

Post a Comment