STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 8, 2014

Mohammed Matumla anaanza tambo dhidi ya Miyeyusho

   Bondia Francic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakikumbatiana baada ya kukubaliana kuzipiga April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba 
****
BONDIA Mohamed Matumla 'Snake JR' ameapa kuwa bondia Francis Miyeyusho 'Chichi Mawe' hatotoka salama siku ya mpambano wao wa Aprili 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam.
Akizungumza kuhusu pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu na watanzania wengi kwa ujumla pamoja na nchi za jirani, Matumla mtoto wa bingwa wa zamani wa dunia, Rashid Matumla 'Snake Man', amesema amekuwa akitafuta kwa muda mrefu sana Miyeyusho lakini hawakupatikana wadhamini wa kuwapambanisha.
Na anashukuru kujitokeza kwa promota Ally Mwazoa kutoka Tanga kwa kujitokeza kudhamini mpambano huo litakalokuwa chini ya TPBO na Rais wake Yassin Abdallah 'Ustadhi', aliyedai amekuwa amekuwa akiwasaidia vijana chipkizi kuibua vipaji vyao na kujulikana katika masumbwi nchini.
"Nimemjua Miyeyusho kwa kuangalia mapambano yake mengi tu aliyopigana na nimemuona ana madhara yoyote hivyo nina uwezo wa kumkabili kikamilifu," alitamba Matumla na kuongeza;
"Nadhani amekuwaakitamba kwa vile hukutana na mabondia wachovu tu, ambao hata mimi nishawahi kukutana nao na kuwachapa vibaya sana, hivyo yeye anachotambia ni kumpiga baba yangu mdogo  Mbwana Matumla," alisema.
Matumla alisema anakumbuka Miyeyusho alimpiga Mbwana mara moja na yeye kupigwa mara mbili ambapo siku akishinda alimpiga mdogo wake (Doyi Miyeyusho) katika pambano la utangulizi.
 
Matumla alisema inawezekana Miyeyusho akaingia kwenye uilingo kwa nia ya kuimlipa kisasi mdogo wake aliyemtwanga kwa KO ya raundi ya pili, lakini akamtahadharisha kuwa atakuwa ulingoni kumlipia kisasi baba yake mdogo.
Alisema anaendelea kufanya mazoezi chini ya kocha ambaye pia ni baba yake Rashidi Matumla na kuahidi  kumpiga Miyeyusho katika pambano hilo litakalosindikizwana michezo mingine kadha ya utangulizi.

No comments:

Post a Comment