Harry Kane akifunga bao la pili la Spurs |
Nyota huyo wa Togo, alifunga mabao yake katika kila kipindi katika mchezo huo uiliochezwa uwanja wa nyumbani wa Spurs, White Hart Lane, la kwanza kwenye dakika ya 28 likiwa la kusawazisha baada ya wageni kuwatangulia kupitia bao la Lee Cattermole aliyefunga dakika ya 17 ya mchezo.
Bao lake la pili alilifunga kwenye dakika ya 86 yakitanguliwa na mabao ya Harry Kane aliyefunga la pili kwa Spurs katika dakika ya 59 na jingine la tatu lililotupiwa kimiani na Christian Eriksen katika dakika ya 78.
Spurs ilihitimisha karamu yake ya mabao dakika za nyongeza kupitia kwa Gylfi Sigurdsson akimaliza kazi nzuri ya Younes Kaboul na kuifanya timu yao ifikishe pointi 59 na kuishusha Manchester United hadiu nafasi ya saba kutokana na kuwazidi pointi mbili. Mashetani Wekundu ambao kesho watakuwa ugenini nchini Ujerumani kupepetana na Bayern Munich katika mechi ya mkondo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wana pointi 57..
No comments:
Post a Comment