WAKATI Climt Dempsey wa Marekani akiweka rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi mpaka sasa kwenye Kombe la Dunia likikamata nafasi ya tano tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 1930, Mjerumani Thomas Muller amewafunika wakali wengine kwa kuongoza orodha ya ufungaji mpaka sasa.
Muller anaongoza msimamo akiwa na mabao matatu aliyioyapata jana wakati wakiiangamiza Ureno kwa mabao 4-0 na kuwazidi Robin Van Persie, Karim Benzema na Arjen Robben, Neymar waliokuwa wakiongoza na mabao mawili kila mmoja wakati raundi ya kwanza ikitarajiwa kumalizka leo kabla ya timu nyingine kuanza ngwe ya pili ya makundi.
Muller alifunga mabao hayo katika pambano la kundi la kifoi ambalo lilishuhudia Mmarekani Clint Dempsey akifunga bao la mapema zaidi katika michuano ya mwaka huu ya nchini Brazili katika sekunde ya 29 tu na kukamata nafasi ya tano katika goli la mapema lililowahi kufungwa kwa muda wote wa michuano hiyo ya Kombe la Dunia.
Bao la Mmarekani huyo limepitwa na yale ya Hakan Sukur linaloongoza likiwa lifungwa Sekunde ya 11 katika michuano ya mwaka 2002, Vaclav Masek aliyefungwa sekunde ya 16 kwenye michuano ya mwaka 1962, Ernst Lehner la sekunde ya 25 kwenye michuano ya mwaka 1934 na lile la Brayan Robson la sekunde ya 27 michuano ya mwaka 1982.
Orodha ya mabao ya mapema katika Kombe la Dunia ni kama ifuatavyo;
Hakan Sukur (2002) Sekunde 11
Vaclav Masek (1962) Sekunde 16
Ernst Lehner (1934) Sekunde 25
Brayan Robson (1982) Sekunde 27
Clint Dempsey (2014) Sekunde 29
Bernard Lacombe (1978) Sekunde 30
Emile Veinante (1938) Sekunde 35
Arne Nyberg (1938) Sekunde 35
Florian Albert (1962) Sekunde 50
Adalbert Desu (1930) Sekunde 50
Chini ni Orodha ya wafungaji wanaoongoza kwa sasa katika michuano ya Brazil;
3- Thomas Müller (Germany)
2- Karim Benzema (France)
Neymar (Brazil)
Arjen Robben (Netherlands)
Robin van Persie (Netherlands)
1- Lionel Messi (Argentina)
Xabi Alonso (Spain)
P. Armero (Colombia)
Mario Balotelli (Italy)
J. Beausejour (Chile)
Winfried Bony (Côte d'Ivoire)
Gervinho (Cote d'Ivoire)
T. Cahill (Australia)
J. Campbell (Costa Rica)
Edinson Cavani (Uruguay)
S. de Vrij (Netherlands)
Andre Ayew (Ghana)
Clint Dempsey (USA)
John Brooks (USA)
Mats Hummels (Germany)
No comments:
Post a Comment