STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, July 18, 2014

Hemed, Senga waonja Pishi la Kajala

MSANII nyota wa filamu nchini Hemed Suleiman anatarajiwa kuonekana katika kazi mpya ya Kajala Masanja iitwayo 'Pishi'.
Filamu hiyo miongoni mwa filamu tatu zilizoandaliwa na mwanadada huyo kupitia kampuni yake ya Kay Entertainment na imewashirikisha wasanii wengine nyota wakiwamo wachekeshaji mahiri nchini Senga, Asha Boko, Tausi na Mzee Onyango.
Akizungumza na MICHARAZO, Kajala alisema tofauti na filamu yake anayotarajia kuiachia hivi karibuni ya 'Laana', ndani ya Pishi ni ucheshi mtupu na yeye mwenyewe akiicheza kikomedi.
"Wengi wanadhani Kajala ni sistaduu aliyezoea kucheza filamu za kimapenzi tu, ndani ya 'Pishi' ni vunja mbavu mwanzo mwisho ikikusanya 'vichwa' adimu kama Asha Boko, Senga, Onyango na wengine," alisema.
Alidokeza filamu hiyo mpya itatoka mwishoni mwa mwezi ujao ili kutoa nafasi ya filamu yake ya 'Laana' iliyoigizwa na wasanii kama Ahmed Salim 'Gabo', Mama Sonia, Mama Kawele na Pastor Myamba kupata nafasi sokoni.

No comments:

Post a Comment