STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, July 18, 2014

Serengeti Boys wapo njema kuwavaa Amajimbos U17

KOCHA Mkuu wa Serengeti Boys, Hababuu Ali Omari amesema morali ya wachezaji wake ipo juu kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) itakayochezwa leo.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 itafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni. 
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam, Kocha Hababuu amesema nia ya kikosi chake ni kuhakikisha wanafika kwenye fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Niger. 
“Tunaiheshimu Afrika Kusini, lakini hatuiogopi. Morali ya wachezaji ipo juu na wanajiamini. Kimsingi wanajua kuwa hii ndiyo njia ya wao kutokea kwenye mpira wa miguu, kwa hiyo lengo ni kushinda,” amesema Kocha Hababuu. 
Naye Kocha wa Afrika Kusini, Molefi Ntseki amesema anaziheshimu timu za Tanzania, na changamoto aliyonayo ni kuhakikisha kuwa anashinda mechi hiyo kwani mara ya mwisho kwa timu yake kushiriki fainali za Afrika ilikuwa miaka sita iliyopita. Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000 na tiketi zitapatikana uwanjani kwenye magari maalumu.

No comments:

Post a Comment