STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, July 18, 2014

UJERUMANI YAKWEA KILELE UBORA DUNIANI, TANZANIA HAIJAMBO

Mabingwa wapya wa Dunia, Ujerumani
MABINGWA wapya wa Dunia, Ujerumani imepaa hadi kileleni mwa viwango vya ubora wa soka duniani ikiwa ni mara ya kwanza kwao katika miaka 20, FIFA ilitangaza jana.
Ushindi wa 1-0 katika mechi ya fainali umewainua hadi nafasi ya kwanza katika orodha ya viwango hivyo, nafasi moja juu ya wapinzani wao wa mechi ya fainali, Argentina, ambao wamepanda kwa hatua tatu hadi nafasi ya pili.
Uholanzi wamepaa kwa hatua 12 hadi kushika nafasi ya tatu kufuatia mwendo wao mzuri uliowashuhudia wakimaliza wa tatu katika Kombe la Dunia nchini Brazil.
Hispania wamelipa gharama ua kushindwa kusonga mbele kutoka katika hatua ya makundi nchini Brazil kwa kuanguka kutoka katika nafasi ya kwanza hadi ya nane, huku Colombia, Ubelgiji na Uruguay zikichukua nafasi za juu yao.
Wenyeji Brazil, waliosambaratishwa kwa magoli 7-1 dhidi ya Ujerumani katika nusu fainali katika matokeo yaliyostua zaidi kwenye michuano hiyo, wameanguka kwa hatua nne hadi kushika nafasu ya saba.
England wameanguka kwa hatua 10 hadi kushika nafasi ya 20 katika orodha hiyo ya viwango, nafasi ambayo ni ya chini zaidi kwao tangu Mei 1996, baada ya mwendo mbaya kwenye Kombe la Dunia ambao vipigo katika mechi mbili za ufunguzi ziliwapa rekodi mbaya zaidi katika miaka 50.
Katika orodha hizo Tanzania imejitoa kimasomaso kwa kukwea kwa nafasi saba kutoka nafasi ya 113 mpaka 106 huku kwa upande wa Afrika nako kukiwa na mabadiliko kwa Algeria kuongoza kwa kuwa katika nafasi ya 24 walikufuatiwa na waliokuwa vina Ivory Coast katika nafasi ya 25.
'Top 10' ya Dunia inaongozwa na 1. Ujerumani, 2. Argentina, 3. Uholanzi, 4. Colombia, 5. Ubelgiji, 6. Uruguay, 7. Brazil, 8. Hispania, 9. Uswisi, 10. Ufaransa.
Tanzania imepaa kwa nafasi hatua 7 hadi kushika nafasi ya 106 duniani wakati wapinzani wao wa Jumapili kwenye kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya kuwania kucheza fainali za Mataifa ya Afrika 2015, Msumbiji nao wakipaa kwa hatua nne hadi kushika nafasi ya 114 duniani.
5-Bora ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati inaongozwa na Uganda inayoshika nafasi ya 87 duniani, Kenya (95, duniani), Tanzania (106), Rwanda (109) na Ethiopia (110).
'Top 10' ya Afrika inaundwa na Algeria inayoshika nafasi ya 24 duniani, Ivory Coast (25, duniani), Nigeria (34), Misri (36), Ghana (38), Tunisia (42), Guinea (51), Cameroon (53), Burkina Faso (58) na Mali wanaoshika nafasi ya 60 duniani.

 

No comments:

Post a Comment