STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 5, 2014

Sheikh mwingine apigwa bomu Arusha


SHEIKH  Sheikh wa Msikiti wa Qiblatan  uliopo eneo la Kilombero jijini Arusha, Sudi Ally Sudi (37)amelipukiwa na bomu la kurushwa kwa mkono nyumbani kwake wakati akila daku na mgeni wake.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka jijini humo na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi, Sheikh Sudi amejeruhiwa sehemu mbalimbali ikiwemo miguu yake yote miwili na sehemu za mapajani pamoja na kifuani na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote miwili.
Akiwa kwenye hospitali ya mkoa Mount Meru, Sheikh Sudi amesema ‘nilijikuta tu nimeumia baada ya kutupwa bomu nyumbani kwangu na kuumia kwenye miguu’
Muhaji Kifea (38) mkazi wa Dar es Slaam aliyekuwa mgeni wa Sheikh huyo alisema "Jana nilikua nimetokea Nairobi hivyo akawa amenitengea chakula nikawa napata daku pale na wakati huohuo ndio bomu likanilipukia na ilikuwa kama saa tano usiku hivi, walilirusha kupitia dirishani na tayari walikuwa na vitisho juu yake, hata kwenye kutupa bomu walitaka kumdhuru yeye siyo mimi"
Hii taarifa imekuja wakati Mufti Issa Bin Shaaban Simba akiwa ametoa tamko juu ya mgogoro wa muda mrefu wa uongozi kwenye msikiti mkuu wa Ijumaa wa mkoa wa Arusha na msikiti mdogo na kuweka wazi viongozi wanaostahili kuiongoza misikiti hiyo kisheria.
Mlipuko huo wa bomu ni wa nne kutokea jijini humo na kushambuliwa kwa Sheikh huyo ni muendelezo wa viongozi wa dini kushambuliwa nchini katika matukio mbalimbali ndani ya jiji hilo na maeneo mengine ya nchini ikiwamo visiwani Zanzibar ambapo masheikh na mapadri wamejikuta wakiuwawa kwa risasi na wengine kumwagiwa tindikali na watu wasiofahamika.

No comments:

Post a Comment