STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 5, 2014

'Mtukutu' Luis Suarez apongezwa kwa uungwana

Suarez aliyepongezwa na Blatter

Rais wa FIFA Sepp Blatter
RAIS wa Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni (FIFA) Sepp Blatter amempongeza mashambuliaji wa Uruguay Luis Suarez kwa uungwana wake wa kumuomba radhi Giorgio Chiellini wa Italia baada ya kufungiwa kwa miezi minne na shirikisho hilo kwa kumng'ata beki huyo kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Blatter, ambaye awali alikataa kuzungumzia kitendo hicho cha ung'ataji au adhabu ya mshambuliaji huyo wa Liverpool, pia amesema ana uhakika kuwa atarejea uwanjani kucheza.
Kashfa ya kung'ata inaelekea haijaathiri jina la Suarez kwenye soko la wachezaji, baada ya Liverpool na Barcelona kuwa katika "mazungumzo mazuri" ya uwezekano wa kuuzwa kwa paundi milioni 80 (sh. bilioni 21.6), na tamko la Blatter si tu litapiga jeki uhamisho huo bali pia kusaidia katika rufaa yoyote ya mchezaji.
Blatter alisema: "Amesema 'Samahani kwa famili ya soka, na hiyo ni fair play. Hiyo inaonyesha ni mchezaji muungwana kiasi gani na nataraji atarudi uwanjani kucheza soka."
Suarez aliomba radhi hadharani wiki iliyopita baada ya kuadhibiwa na FIFA. Kifungo hicho kirefu - ambacho pia kinajumuisha kutocheza mechi tisa za timu ya taifa - kilishutumiwa na baadhi, hasa nchini kwake Uruguay, na Chiellini mwenyewe amedai adhabu ya mshambuliaji huyo ni kubwa mno.
Kutolewa kwa nchi hiyo kwenye michuano hiyo katika hatua ya mtoano na Costa Rica, huku Suarez akiwa amefungiwa, kulimfanya rais wa nchi hiyo kuishutumu FIFA lakini Blatter amekataa kujibu matamshi ya Jose Mujica.

No comments:

Post a Comment