STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 5, 2014

Brazil, Ujerumani Nusu Fainali, James atupia bao Colombia ikiaga

James Rodriguez akishangilia bao lao dhidi ya Brazil, hata hivyo Colombia iliaga mashindano
Kashkash za pambano la Colombia na Brazil
David Luis akishangilia bao lililoiepeleka Brazil Nusu Fainali

Mats Hummels akishangilia bao lake lililoivusha Ujerumani Nusu Fainali za Kombe la Dunia
WAKATI Brazil ikifanikiwa kuifuata Ujerumani kwenye mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2014, mshambuliaji nyota wa Colombia James Rodriguez amejichimbia kileleni mwa Wafungaji Bora wa michuano hiyo akifikisha bao la sita.
Rodriguez ambaye timu yake iling'olewa kwenye michuano hiyo na wenyeji Brazil usiku wa kuamkia leo kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1, amewapa mtihani nyota waliosalia kwenye michuano hiyo kumfukuzia kwenye kuwania kiatu cha dhahabu.
Mshambuliaji huyo wa Monaco alifunga bao la kufutia machozi la Colombia dakika ya 80 kwa mkwaju wa penati, bao ambalo hata hivyo halikusaidia na hivyo kurudi kwao.
Wenyeji walitangulia kupata bao la mapema katika dakika ya 7 kupitia nahodha Thiago Silva akimaliza pasi ya Neymar ambaye alishindwa kumaliza mchezao huo kutokana na kukimbizwa hospitali kwa kuchezwa rafu mbaya na beki wa Colombia Camilo Zuniga aliyemvamia eneo la mgongoni na kumjeruhi eneo hilo.
Bao lililidumu hadi wakati wa mapumziko licha ya kosa kosa za hapa na pale na katika kipini cha pili  wenyeji walizidi kucharuka na kufanikiwa kuongeza bao la pili lililowahakikishia kutinga Nusu Fainali kupitia kwa beki David Luiz katiia dakika ya 69.
Ushindi huo wa wenyeji umewafanya sasa kuvaana na Ujeruman siku ya Jumanne baada ya mabingwa hao wa zamani kuifumua Ufaransa kwa bao 1-0 katika mechi iliyochezwa mapema saa 1 usiku.
Bao pekee lililowapeleka wakali hao katika hatua hiyo lilitumbukizwa kimiani na beki Mats Hummels katia dakika ya 12 na kudumu hadi mwisho licha ya Ufaransa kucharuika kutaka kulisawazisha na kukutana na kikwazo cha kipa Manuel Neuer.
Timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia tangu walipoumana kwenye mechi ya fainali za mwaka 2002 ambapo Ujerumani ilikubali kichapo cha mabao 2-0 ya Ronaldo yaliyoipa Brazil ubingwa wao wa mwisho tangu hapo.

No comments:

Post a Comment