STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 5, 2014

Pigo! Neymar kukosa mechi zote zilizosalia za Kombe la DuniaSTAA wa timu ya Brazil, Neymar hataendelea na michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kuvunjika mfupa unaoshikana na uti wa mgongo wakati wa mechi yao na Colombia usiku wa kuamkia leo.
 Mshambuliaji huyo wa Barcelona amefunga mabao manne katika fainali za mwaka huu, lakini alishindwa kuongeza dhidi ya Colombia kabla ya kutolewa nje kwa machela dakika tatu kabla ya mechi kumalizika.
Kocha wa Brazil Luiz Felipe Soclari alisema: “Sidhani kama ataweza kucheza mechi ijayo”.
“Amekimbizwa hospitali binafsi na madaktari kwasababu aligongwa na goti katika mgongo wake”.
” Alikuwa analia kwa maumivu. Haitakuwa rahisi kwake kuimarika kwa kuzingatia ukweli kwamba ni majeruhi ya mgongo na maumivu aliyonayo ni makubwa. Acha tuwe na matumaini kuwa kila kitu kinakwenda vizuri”.
 
Neymar akitolewa nje ya uwanja wakati wa Robo Fainali dhidi ya Colombia.
Staa huyo mwenye mabao manne mpaka sasa kwenye michuano hiyo, alitolewa uwanjani dakika tatu kabla ya mechi yao dhidi ya Colombia kumalizika.

 
Neymar akiwa chini baada ya kuvunjika mfupa.
Katika mechi hiyo, Brazil walishinda mabao 2-1 na kutinga Nusu Fainali ambapo watakutana na Ujerumani Julai 8 mwaka huu.

 
Hivi ndivyo Neymar alivyoumizwa na Zuniga
Kwa mujibu wa taarifa za daktari wa timu ya Brazil, Neymar atakaa nje kwa takribani wiki nne.

 
Neymar akipatiwa huduma ya kwanza.
 
Wapenzi wa soka nchini Brazil wakiwa nje ya hospitali aliyopelekwa Neymar

No comments:

Post a Comment