STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 5, 2014

Stars majaribuni tena leo Bostwana

BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 4-2 toka kwa wenyeji wao Botswana, timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo inatarajiwa kujiuliza tena wakati itakapovaana na Lesotho katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa mjini Gaborone.
Stars ipo Botswana kujiandaa na mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili dhidi ya Mamba ya Msumbiji kuwania kucheza Fainali za Afrika za mwakani zitakazochezwa nchini Morocco.
Timu hiyo inayonolewa na kocha Mart Nooij, inashuka dimbani kuivaa na Lesotho ikiwa ni siku chache tangu inyukwe mabao 4-2 na Botswana katika moja ya mechi zake za kujiwinda na pambano la Mamba litakalochezwa Julai 20 jijini Dar es Salaam.
Hiyo ni mechi ya kwanza kwa timu hizo kukutana na mara baada ya mchezo huo Stars itarejea nchini kuendelea na kambi wakati wapinzani wao watakuwa wakijiandaa na mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya wenyeji wao Botswana kabla ya kuwasubiri Kenya katika mechi ya kuwania fainali za Afrika 2015.

No comments:

Post a Comment