WAZIRI mkuu nchini Senegal Aminata 'The Iron Lady' Toure ameachishwa kazi baada ya chama tawala kushindwa katika uchaguzi mkuu.
Maafisa wanasema kuwa Rais Macky Sall alimtaka Mwanamama huyo kujiuzulu baada ya kuhudumu chini ya kipindi cha mwaka mmoja.
Waandishi wanasema kuwa kutorodhika kwa wanachi
kuhusu sera za uchumi za serikali hiyo ndio sababu kuu ya chama hicho
kushindwa katika uchaguzi huo.
Waziri Mkuu huyo alikuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo nchini humo tangu Mame Madior Boye kuweka rekodi alipochaguliwa mwaka 2001 na kudumu kwa kipindi kifupi chini ya utawala wa Abdoulaye Wade.
BBC
No comments:
Post a Comment