STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 15, 2014

Coast Modern kuwatoa watatu wapya

Omar Tego
KUNDI la muziki wa taarab la Coast Modern 'Watafiti wa Mipasho' limefanikiwa kuwapata wasanii watatu wapya chipukizi wanaiotarajia kuwatambulisha na kazi zao mpya wanazotarajia kuzirekodi hivi karibuni.
Chipukizi hao walionyakuliwa na kundi hilo linaliotamba kwa sasa na wimbo wa 'Katiba Mpya' ni Mwajuma Othman, Aisha Abdallah na Dualla Ally ambao wameanza mazoezi ya nyimbo zao kabla ya wiki mbili zijazo kuingia studio kuzirekodi.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Omar Tego 'Special One' aliiambia MICHARAZO kuwa, wasanii hao wapya wana vipaji vikubwa vya kuimba na kuwatabiria kuja kufunika mbeleni mara baada ya kazi zao wanazoziandaa kurekodi kuanza kurushwa hewani.
Tego alisema tayari kila msanii ameshatungiwa wimbo wake na kuufanyia mazoezi kwa sasa na wataingia kuzirekodi kabla ya kuachiwa hewani wakati akijipanga kutengeneza video zake.
"Tuna vijana watatu wakali achaa...wawili wa kike na mmoja wa kiume na kwa sasa wapo katika mazoezi makali ya nyimbo zao kabla ya kuingia studio kuzirekodi," alisema Tego.
Kundi hilo limejipatia umaarufu mkubwa katika miondoko ya taarab kutokana na nyimbo kadhaa kama 'I'm Crazy for U', 'Kupenda Isiwe Tabu', Chongeni Fenicha', Mwanamke Kujiamini', 'Damu Nzito', 'Gubu la Mume' na nyingine.

No comments:

Post a Comment