STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 15, 2014

YANGA YAIPIGA BAO SIMBA, YAMNASA BEKI WA JKT RUVU

Guu la kushoto; Yanga SC imeizidi kete Simba SC katika saini ya Edward Charles
YANGA SC imefanikiwa kumpata beki chipukizi wa JKT Ruvu, Edward Charles baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wake kutoka timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa na kumsainisha Mkataba wa miaka mitatu.
Yanga SC kwa miezi miwili sasa imekuwa ikisotea saini ya mchezaji huyo kwa kuanzia kufuata taratibu za kuvunja mkataba wake jeshini- hadi leo ilipokamilisha. Viongozi wa Yanga SC wakiongozwa na Francis Kifukwe leo walikuwa na kikao cha mwisho na uongozi wa JKT juu ya suala la uhamisho wa mchezaji huyo na mambo yamekwenda vizuri. Beki huyo alikuwa pia anawaniwa na mahasimu Simba SC, ambao jitihada zao ziligonga ukuta mapema, baada ya kuambiwa wapinzani wao Yanga SC, wamepiga hatua kubwa katika kufukuzuia huduma za chipukizi huyo. Edward sasa atajiunga na Yanga SC mara moja chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo kuanza maandalizi ya msimu mpya. Ni Maximo aliyewasukuma viongozi wa Yanga SC kufukuzia haraka saini ya mchezaji huyo baada ya kutovutiwa na uchezaji wa beki wa sasa wa kushoto wa klabu hiyo, Oscar Joshua.  Edward Charles ni kati ya chipukizi waliopo timu ya taifa ya wakubwa kwa sasa, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij ambao wanainukia vizuri.   Ni mkabaji mzuri, ana nguvu, kasi- mbinu za anapokuwa na mpira na asipokuwa nao na pia hupanda vizuri kushambulia na kurudi kwa haraka. Anasifika kwa kupiga krosi nzuri pamoja na mpira iliyokufa.
BIN ZUBEIRY

No comments:

Post a Comment