STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 15, 2014

Snura kukirudia Kigoda chake cha zamani!

Snura katika pozi
STAA wa nyimbo za 'Majanga', 'Umevurugwa' na 'Umeshaharibu', Snura Mushi, amesema yupo katika mipango ya kuurudia wimbo wake wa zamani uitwao 'Kigoda'.
Wimbo huo wa 'Kigoda', ulirekodiwa na Snura miaka zaidi ya 15 iliyopita wakati akianza kuibukia kwenye sanaa, lakini haukupata nafasi ya kumtambulisha kama kazi zake za sasa.
Akizungumza na MICHARAZO, Snura alisema ataurudia wimbo huo kwa kuuweka kwenye miondoko ya mduara akiamini utakubalika kwa vile ni wimbo uliokuwa na mistari iliyoshiba na yenye ujumbe mzuri.
Snura alisema kazi hiyo itafanywa mara baada ya kutengeneza video za nyimbo zake mbili zilizokamilika kwa sasa za 'Ime-expire' na 'Mtaka Basi' ambazo bado hazijaachiwa hewani.
"Nipo katika mpango wa kuurudia wimbo wangu kwa kwanza kabisa katika fani ya muziki uitwao 'Kigoda', ila kazi hiyo itafanywa baada ya kukamilisha video ya nyimbo zangu mpya za sasa," alisema Snura.
Msanii huyo ambaye pia  ni muigizaji wa filamu alisema kila uchao yeye huwaza namna ya kuwashushia mashabiki wake burudani kama njia ya kuwashukuru kwa kumpokea vyema katika fani hiyo.

No comments:

Post a Comment