STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 15, 2014

Tanzania yaporomoka FIFA, yashindwa hata na Sierra Leone

Kikosi cha Stars ambacho kiling'olewa michuanoni na Msumbiji na kuporomoka kwenye viwango vipya vya FIFA
TANZANIA imeporomoka kwa nafasi nne katika viwango vya soka vilivyotolewa na Shirikikisho la Soka duniani, Fifa.
Katika viwango hivyo ambavyo Ujerumani imeendelea kuongoza kwa ubora duniani ikifuatiwa na Argentina na Uholanzi, Tanzania imeshika nafasi ya 110 huku Msumbiji ambayo iliitoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco ikipanda kwa nafasi saba na kuwa ya 107.
Kwa upande wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imeendelea kuwa kinara ikipanda nafasi sita na kuwa ya 81 duniani ikifuatiwa na Rwanda ambayo ni ya 101 baada ya kupanda nafasi nane, Kenya inafuata ikiwa ni 104 licha ya kushuka nafasi tisa mwezi huu, huku Burundi ikiburuza mkia ikiwa ni ya 129 baada ya kushuka nafasi tatu.
Barani Afrika kwa ujumla, Algeria inaongoza huku kidunia ikishika nafasi ya 24 ikifuatiwa na Ivory Coast (25), Nigeria (33), Ghana (36) na Misri (38).
Chini ni 20 Bora ya Dunia safari hii ambayo inafungwa dimba na England;
1. Ujerumani,
2. Argentina
3. Uholanzi
4. Colombia
5. Ubelgiji
6. Uruguay 
7. Hispania
7. Brazil
9. Uswisi
10. Ufaransa
11. Ureno
12. Chile
13. Ugiriki
14. Italia
15. Costa Rica
16. Croatia
17. Mexico
18. Marekani
19. Bosnia and Herzegovina
20. England
AFRIKA 20 Ipo hivi:
    
1. Algeria
2. Ivory Coast
3. Nigeria
4. Ghana
5. Misri
6. Tunisia
7. Sierra Leone
8. Cameroon
9. Burkina Faso
10.Senegal
11.Mali
12.Libya
13.Guinea
14. Afrika Kusini
15.Cape Verde
16.Angola
17.Benin 
18. Kongo
19. Morocco
20. Uganda

No comments:

Post a Comment