STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 15, 2014

MAMIA WAMZIKA MAMA TUNDA WA AFANDE SELE

 Professor akiwa na Afande Sele Morogoro
 Professor Jay amesafiri hadi mkoani Morogoro kwenda kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wa msanii mwenzake Afande Sele.
Kupitia Instagram, Professor ameshare picha akiwa kwenye mazishi na kuandika: Msibani Morogoro nyumbani kwao marehemu Asha au mama Tunda sasa hivi… tunajiandaa kwenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele saa kumi jioni ya leo, bwana alitoa bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe….Amen
Jeneza la marehemu likiwa nje pamoja na watu mbalimbali waliojitokeza katika mazishi hayo
Awali Afande Sele alisema kifo cha Mama Tunda kimetokana na uzembe wa madaktari. Mama Tunda alifariki baada ya kulazwa kutokana na kuugua Malaria. Akizungumza na Bongo5 leo, Afande alidai kuwa bila uzembe wa madaktari huenda malaria isingechukua uhai wa Mama Tunda.

Afande Sele akilia kwa uchungu
“Mama Tunda ametuachia pengo kubwa sana kwenye familia,” alisema Afande. 
 “Amefariki jana saa tano usiku katika hospitali kubwa hapa Morogoro kutokana na uzembe wa madaktari. Walimpa matibabu akarudi nyumbani, sitaki kulizungumzia kiundani kwa sasa hivi kwa sababu tupo kwenye wakati mgumu. 
Huku mazishi yatafanyika kuanzia kama saa tisa hivi lakini bado hatutajua itakuwa wapi bado tupo kwenye mipango. Malaria ilimchukua sana, kwa familia na watoto kwetu ni msiba mkubwa sana, yaani ni huzuni sana,” aliongeza.
MAMIA ya wakazi wa mkoa wa Morogoro na wasanii wa fani mbalimbali jana walijitokeza katika mazishi ya mke wa nyota wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi 'Afande Sele' yaliyofanyika katika makaburi ya Kola katika Manispaa ya Morogoro.
Mke wa Afande Sele, Asha Shengo maarufu kama Mama Tunda alifariki usiku wa kuamkia Alhamisi majira ya saa 5.45 katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro alikokuwa akitibwa baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria iliyomuanza siku ya Jumatatu.
Akizungumza kabla ya mazishi hayo, mmoja wa ndugu wa marehemu, Ally Bushiri alisema Mama Tunda alianza kujisikia vibaya siku ya Jumatatu na kwenda kupimwa na kubainika alikuwa na malaria nne.
Alisema kuwa baadaye Mama Tunda alipatiwa matibabu na siku ya Jumanne hali yake haikuwa nzuri na kupelekwa katika hospitali ya Mtakatifu Mary iliyopo eneo la la kata ya Mafiga na ilipofika Jumatano asubuhi hali yake iliimarika na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Bushiri alisema kuwa siku ya Jumatano jioni hali ya Mama Tunda ilibadilika na hivyo ndugu waliamua kumpeleka katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako alianzishiwa matibabu na wakati akiendelea na matibabu ghafla ilipofika majira ya saa 5.45 hali ilibadilika na kufariki dunia.
Akizungumza kwa uchungu, msanii Afande Sele alisema kuwa marehemu Mama Tunda amemuachia pengo kubwa hasa watoto wake wawili Tunda pamoja na Asante, mwenye umri wa miaka mitatu .
Afande Sele ambaye muda wote alionekana kububujikwa na machozi alisema kuwa mpaka sasa anashindwa kuamini kama mzazi mwenzake huyo ametangulia mbele za haki kwakuwa ndiyo alikuwa mmoja wa washauri wa karibu katika mambo yake ya muziki.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa Afande Sele, Nickson Mkilanya akimuelezea marehemu Mama Tunda alisema kuwa alikuwa ni miongoni mwa wanawake shupavu, mvulivu na mwenye kupenda ushirikiano katika kila jambo.
Mungu alaze roho ya marehemu Mama Tunda mahali pema poponi Amina.
 

No comments:

Post a Comment