STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 5, 2014

van Persie atatahadharisha Falcao Old Trafford

http://i4.eurosport.com/2014/09/03/1306699-28127090-640-360.jpgRADAMEL Falcao hajahakikishiwa namba katika kikosi cha kwanza cha Manchester United, kwa mujibu wa mshambuliaji wa Mashetani Wekundu, Robin van Persie.
Mchezaji wa kimataifa wa Colombia, Falcao (28), alijiunga na Man  U kwa mkopo wa mwaka mmoja uliowagharimu paundi milioni 6.
"Nakaribisha ujio wake, anatufanya tuwe bora zaidi," Van Persie aliiambia Fox Sports NL.
"Katika klabu kubwa daima unahitaji wachezaji bora, ambao pia wanafiti katika falsafa. Falcao ni lazima apiganie namba, kama ilivyo kwangu mimi."
Falcao alifunga magoli 11 katika mechi 20 alizochezea klabu ya Monaco ya Ligi Kuu ya Ufaransa msimu uliopita, kabla ya kuumia goti Januari, maumivu yaliyomweka nje ya Kombe la Dunia nchini Brazil.
Kulikuwa na uvumi kwamba ameletwa Man U ili kuchukua nafasi ya Van Persie (3)1, ambaye amevumishiwa kuhitaji kufanyiwa upasuaji wa goti.
"Nimevutiwa kwamba watu wamefikiria kitu kama hicho," alisema Mholanzi huyo, ambaye alitua Old Trafford akitokea Arsenal kwa paundi milioni 24 mwezi Agosti 2012 na alifunga magoli 26 ya ligi katika msimu wake wa kwanza na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa.
"Sijui yametokea wapi hayo na naweza kusema huku mkono wangu nikiwa nimeuweka kwenye moyo wangu kwamba sitakuwa hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji."

No comments:

Post a Comment