STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, December 6, 2014

Kocha Kibadeni azushiwa kifo

http://4.bp.blogspot.com/-JyS7nbpnrcc/Ucfjy4uGMhI/AAAAAAAAG6U/hFNox8pcBys/s1600/Kinesi.jpgKOCHA na nyota wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Abdallah ‘King’ Kibadeni amezushiwa kifo na kusababisha utata mkubwa.
Taarifa ziliripotiwa na mtandao mmoja zimefanya watu waanze kumpigia simu kila mara, na wengine kuipigia MICHARAZO kutaka ufafanuzi ambao hata hivyto ilikuja kubainika kuwa ni uongo.
Kocha huyo aliyewahi kuwa nyota wa klabu za Simba na Majimaji na Taifa Stars alisema hajui aliyezua jambo hilo alikuwa na lengo gani kwani limempa usumbufu yeye na watu wengine.
"Mimi ni mzima buheri, siumwi wala sijapata ajali wala jambo lolote baya na sijui aliyefanya hivi alikuwa na lengo gani, ila nadhani ni uhuru uliopo sasa kuanzia mitandao ya kijamii," alisema na kuongeza;
“Kweli hata mimi napigiwa simu na watu wengi sana kama nimefariki dunia, hawa watu sijui wamepata wapi hizi taarifa.
“Kweli siku chache zilizopita nimefanyiwa upasuaji wa jicho. Hadi sasa niko safi kabisa, ninaendesha hata gari.
“Kupitia mtandao wako, naomba niseme hivi; ninawaomba radhi wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizi,” alisema Kibadeni na kuongeza.
“Ila ninaomba wale ambao wanaopata taarifa ni vizuri kuzihakikisha kuliko kusababisha usumbufu kwa watu.”

No comments:

Post a Comment