STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, December 6, 2014

Arsenal yafa ugenini, Spurs, Liverpool zang'ang'aniwa

Stoke's Peter Crouch recreates the 'Cristiano Ronaldo' celebration for his goal
Crouch akishingalia bao lake la mapema dhidi ya Arsenal
Ryan Mason and Marouane Chamakh
Vita ya Spurs na Crystal ilikuwa hivi
Steven Gerrard
Nahodha Steven Gerrard akiipigiania LIverpool akitokea benchi bila ya mafanikio
Charlie Austin
QPR ilipotakata nyumbani
SAA chache baada ya vinara wa Ligi Kuu ya England Chelsea kunyukwa ugenini ikiwa ni kwa mara ya kwanza, Arsenal nayo imekumbana na aibu kama hiyo ugenini baada ya kulala mabao 3-2 kwa Stoke City.
Dalili mbaya kwa Arsenal zilianza mapema baada ya kufungwa bao la kushtukiza dakika moja tu tangu kuanza kwa pambano hilo wakati Peter Crouch alipoiandikia Stoke bao la kuongoza akimaliza kazi ya Mamme Diouf.
Dakika ya 35 Bojan aliiongezea wenyeji bao kabla ya kumegewa pande na Jonathan Walters, ambaye alifunga bao jingine la Stoke lililokuwa la tatu sekundu chache kabla ya mapumziko.
Vijana wa Arsene Wenger walirejea kwa kasi katika kipindi cha pili kwa kuanza kurejesha mabao hayo, baada ya Santi Cazorla kuandika bao dakika ya 68 kwa penati kabla ya Aaron Ramsey kuongeza dakika mbili baadaye akimalizia kazi ya Alexis Sanchez.
Arsenal ilijikuta ikimpoteza beki wake Calum Chembers baada ya kuonyesha kadi ya pili ya manjano iliyoambatana na nyekundu.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Liverpool ikiwa nyumbani iling'ang'aniwa na Sunderland na kutoka suluhu sawa na ilivyokuwa kwa Tottenham Hotspur iliyoshikiliwa na Crystal Palace na Hull City kushindwa kutoshana nguvu na Wes Bromwich Albion kwa kutoka pia suluhu huku QPR ikipata ushindi wake wa pili kati ya mechi zake tatu za karibuni.
Kwa hivi sasa mabaingwa watetezi Manchester City wapo dimbani kuumana na Everton katika pambano linalochezwa uwanja wa Etihad.
Jumatatu kutakuwa na pambano moja la kukata na shoka kati ya Southampton itakayoialika Manchester United ambayo inasaka kuingia kwenye Tatu Bora.

No comments:

Post a Comment