STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, December 6, 2014

Yanga yaidonyoa Express, Maximo amficha Emerson

Emerson (wa pili kulia) akiwa na Hussen Javu, Kiiza na Coutinho
IKICHEZA bila kiungo mkabaji mpya toka Brazil, Yanga imetuma salamu kwa watani zao Simba baada ya kuifunga Express ya Uganda kwa bao 1-0 katika pambano la kirafiki la kimataifa lililochezwa uwanja wa Taifa.
Bao pekee lililoizamisha Express ambao jana walilazimishwa suluhu na Simba katika pambano jingine la kirafiki la kimataifa liliwekwa kimiani na Mganda, Hamis Kiiza 'Diego' katika dakika za lala salama na kuzima ndoto za Waganda wenzake kuambulia suluhu katika mchezo huo.
Kiiza aliyeingia uwanjani toka benchi alifunga bao hilo kwa shuti baada ya kuunganisha krosi ya Simon Msuvah, na mashabiki waliofurika uwanjani walikosa uhondo kwa kushindwa kumuona Emerson Oliveira ambaye kocha Marcio Maximo aliamua kutompanga kabisa ili kuficha makali yake kabla ya kuvaana na Simba Jumamosi ijayo kwenye mechi ya Bonanza ya Nani Mtani Jembe.

No comments:

Post a Comment