STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, May 27, 2016

Kaka akumbukwa Brazil, aitwa kuziba pengo la Costa

http://www.fantasista10.co.uk/wp-content/uploads/2015/03/Kaka-orlando1.jpg
Kaka akiwajibika kwa klabu yake ya Orlando
BADO wamo. Straika mkongwe wa Brazil anayeichezea klabu ya Orlando City, Kaka ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi yake kwa ajili ya michuano ya Copa America akichukua nafasi ya Douglas Costa.
Costa mwenye umri wa miaka 25, amepata majeraha ya misuli ambayo yatamfanya akose michuano hiyo maalumu ya kuadhimisha miaka 100 toka kuanzishwa kwake. Kaka mwenye umri wa miaka 34 ameichezea Brazil mechi 91 na kufunga mabao 29 katika kikosi hicho.
Costa alikuwa sehemu ya kikosi cha Bayern Munich ambacho kimeshinda taji la Bundesliga na Kombe la Ujerumani katika msimu wa mwisho wa Pep Guardiola na timu hiyo.
Brazil imepangwa kufungua pazia la Copa America kwa kucheza na Ecuador katika Uwanja wa Rose Bowl huko Pasadena, California Juni 4 mwaka huu, huku mechi zao nyingine mbili za kundi B zitakuwa dhidi ya Haiti na Peru.

No comments:

Post a Comment