STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, May 27, 2016

Ronaldo kwa vijembe hajambo, awakejeli Barcelona kimtindo

http://u.goal.com/2890500/2890552.jpgHEBU msikieni CR7. Straika nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya itakuwa na thamani kubwa zaidi kuliko mataji mawili yaliyonyakuliwa na wapinzani wao, Barcelona msimu huu.
Ronaldo aliye na umri wa miaka 31 aliyekuwa majeruhi katika wiki za karibuni na kumfanya akose mechi ya nusu fainali ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City ni kama amewapiga kijembe wapinzani wao hao.
Hata hivyo juzi aliwaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo akidai kuwa atakuwa fiti kwa asilimia 100 kwa ajili ya fainali hiyo dhidi ya Atletico Madrid.
Akihojiwa Ronaldo amesema kama wakishinda taji hillo la Ligi ya Mabingwa itakuwa ni thamani kubwa zaidi kwao kuliko mataji mawili ya Barcelona waliyoshinda hivi karibuni, kwani taji la michuano hiyo ya Ulaya liko katika ndoto za kila mchezaji. Klabu hasimu za jiji la Madrid, Real Madrid na Atletico Madrid zitakutana kesho Jumamosi katika fainali ya tatu zilizozikutanisha timu za Hispania na mechi ya fainali ya pili baina yao baada ya mwaka juzi 2014 kukutana na Real kushinda 4-1.

No comments:

Post a Comment