STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, May 27, 2016

Ufaransa yaapa fainali za Euro 2016

http://gdb.voanews.com/23C9424D-B2D5-4DD1-BDCC-2F282A62DD35_cx23_cy23_cw62_w987_r1_s_r1.jpgUTAWALA wa nchi ya Ufaransa umesema kuwa inatarajia kuweka polisi zaidi ya 60,000 ili kulinda usalama katika michuano ya Euro 2016 itakayopanza Juni 10 wakiapa kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha wanazuia shambulio lolote la kigaidi katika kipindi chote cha mashindano hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, Bernard Cazeneuve ndiye aliyetoa kauli hiyo baada ya Uwanja wa Ufaransa uliopo jijini Paris ambao ndio utatumika kwa ajili ya mechi ya ufunguzi na fainali, kuleta rabsha Jumamosi iliyopita kabla ya fainali ya Kombe la Taifa.
Moshi mkubwa uliohisiwa kuwa bomu ulilipuka ndani ya uwanja na kusababisha mashabiki kuchanganyikiwa na kukimbia hovyo kuelekea milango ya kutoka nje ya uwanja.
Akihojiwa Waziri huyo amesema tukio la Jumamosi iliyopita halihusiani na maandalizi yao kwani waandaaji walikuwa tofauti.
Waziri huyo aliongeza kuwa katika michuano ya Euro 2016 inayotarajiwa usalama utakuwa ni kipaumbele chao cha kwanza ili kuhakikisha hakuna tukio lolote hatarishi ya kigaidi litakaloweza kutokea.

No comments:

Post a Comment