STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, May 27, 2016

Yanga yaibania Simba kucheza kimataifa

Yanga
Simba
 MWAKA wa hasara ni wa hasara tu. Baada ya ndoto za kucheza fainali za michuano ya Nile Basin iliyopangwa kufanyika Sudan kupotea hewani, Simba imeikosa tena fursa nyingine ya kushiriki michuano ya kimataifa mwaka huu.
Simba ilikuwa ikijipa matumaini ya kuwemo kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyopangwa kufanyika kuanzia mwezi ujao nchini, lakini michuano hiyo sasa haitafanyika tena Tanzania baada ya TFF kuchomoa kuiandaa.
Shirikisho hilo la Soka Tanzana, limetangaza kutoandaa michuano hiyo  inayohusisha timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama ilivyopendekezwa.
Sababu za TFF ya kutoandaa fainali hizo ni kwa kubanwa na ratiba ya michuano ya kitaifa na kimataifa.
Awali mkutano mkuu wa CECAFA, uliamua Zanzibar iwe mwenyeji wa michuano ya Kagame.
Baadaye kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa ilionekana Zanzibar hawataweza kufanya.
Baada ya hapo TFF ilianza kuangalia uwezekano wa mashindano haya kwa kumshirikisha mabingwa wa 2015/16 ambao ni Yanga.
Kutokana na ratiba ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), kipindi ch Juni hadi Agosti, 2016 Yanga watakuwa na kwenye michuano ya CAF hatua ya makundi hivyo ushiriki wao CECAFA utakuwa mgumu ilihali michuano ya CECAFA imepangwa kufanyika Juni na Julai, mwaka huu.
Watetezi wa taji hilo ni Azam na tayari Yanga ilikuwa ikisita kushiriki na kutoa nafasi kubwa kwa Simba kubeba jukumu, lakini kwa hali ilivyo watabidi wasubiri sana.

No comments:

Post a Comment