STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 22, 2013

GOLDEN BUSH USO KWA USO NA CLOUDS FC


Kikosi cha Golden Bush Veterani wakiwa na kocha wao, Madaraka Selemani.

WAKALI wa kutatandaza soka mkoa wa Dar es Salaam, Golden Bush Veterani jioni ya leio inatarajiwa kushuka dimbani kuvaana na kikosi cha kituo maarufu cha redio nchini Cloud's Fm, 'Clouds Fc.
Pambano hilo la kirafiki ambalo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wa jijini kutokana na tambo za pande zote mbili litachezwa kwenye uwanja wa Tanganyika Packers kuanzia saa 10:30 jioni.
Kwa mujibu wa Mlezi wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' ni kwamba kikosi chao tangu Jumatatu walikuwa kambini katikati ya jiji wakijiandaa na pambano hilo baada ya kupoteza mechi yao mwishoni mwa wiki dhidi ya Survey ya Chuio Kikuu.
Ticotico alisema katika mechi ya leo wanatarajia kuwashusha dimbani wachezaji wake nyota ili kuhakikisha wanaitoa nishai Clouds, aliodai walikuwa wakiwakwepa mara kwa mara wakiomba nafasi ya kucheza nao.
"Tupo kamili kwa ajili ya kutoa kipigo kwa Clouds, hasa ikizingatiwa wamekuwa wakitukwepa mara nyingi, pia tumetoka kupoteza mechi mwishoni mwa wiki iliyopita, hivyo hatutaki tena tufanye makosa," alisema Ticotico ambaye ametamba atakuwepo dimbani kuwaongioza vijana wake kusaka ushindi.
Baadhi ya nyota wa timu hiyo wanaotarajiwa kushuka dimbani leo ni pamoja na Wisdom Ndhlovu, Herry Morris, Majaliwa, Said Swedi 'Panucci', Shija Katina, Waziri Mahadhi 'Mandieta' na wengineo, huku wapinzani wao wakitarajiwa kuwategemea zaidi akina Shafii Dauda, Mbwiga Mbwiguke, Lwambano, Ally Mayay 'Tembele', Gofrey Lea na wengineo

Kemmy atamba 'Nguvu ya Imani' ni rasharasha tu

Kemmy katika pozi
MSANII wa zamani wa kundi la Kaole Sanaa, Juliet Samson 'Kemmy', amesema kazi yake mpya anayotarajia kuiingiza sokoni ya 'Nguvu ya Imani' ni mwanzo wa kurudi kwenye 'gemu' baada ya mashabiki wake kumkosa kwa muda mrefu.
Alisema amevunja ukimya kwa kupakua filamu hiyo aliyowashirikisha wasanii kadhaa wanaotamba nchini ili kuthibitisha kuwa bado wamo, tofauti na watu wanavyodhani kuwa enzi zake zimeisha.
"Hizi ni salamu na mvua za rasharasha tu, kuna makubwa yanakuja ndani ya 2013 baada ya 'Nguvu ya Imani'," alisema Kemmy.
Kemmy ambaye ni mtunzi, muandaaji na muongozaji kwa sasa, alisema zipo kazi nyingine zilizokaa tayari kuachiwa mara zitakapokamilika, lakini amefungua pazia na filamu hiyo ambayo hivi karibuni itakuwa mtaani.
Filamu hiyo inayohusu simulizi la wanawake wa jamii ya wafugaji na aina ya misukosuko wanayokumbana katika maisha yao ya kila siku ameiigiza yeye (Kemmy),  Simon Mwapangata maarufu kama 'Rado', Jackson Kabigili na wengine.