STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, March 8, 2013

Spurs yainyuika Inter, Chelsea yachezea kidude ugenini

Garreth Bale akifunga bao la kwanza la Tottenham jana dhidi ya Inter Milan

TIMU ya soka ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza jana iliendelea kufanya vema katika harakati zake za kuwania ubingwa wa Ligi Ndogo ya Ulaya baada ya kuinyuka Inter Milan ya Italia mabao 3-0 wakati 'ndugu' zao wa London, Chelsea wakinyukwa bao 1-0 na Steaua Bucurest katika michuano hiyo.
Mabao mawili ya kipindi cha kwanza kupitia kwa winga mahiri, Garreth Bale  katika dakika ya sita na lile la Gylfi Sigurdsson la dakika ya 18 na la kipindi cha pili kupitia beki wao, Jan Verlonghen yalitosha kuipa nafasi kubwa ya Tottenham kunusa robo fainali ya michuano hiyo kwa msimu huu.
Katika mechi nyingine zilizochezwa usiku wa jana katika mechi hizo kuwania kutinga robo fainali, Chelsea walidunguliwa bao 1-0 ugenini na Steaua Bucurest, huku Newcastle United ililazimisha suluhu ugenini dhidi ya matajiri wa Urussi, Anzhi Makhachkala.
Viktoria Plzeň ilikubali kipigo nyumbani kwao kwa kulazwa bao 1-0 na Fenerbahçe, Lazio ya Italia ikapata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Stuttgart  ya Ujerumani,huku Levante ikiwa nyumbani Hispania ililazimishwa suluhu na Rubin Kazan.
Mechi nyingine ilishuhudiwa Basel  ikiinyuka Zenith mabao 2-0, na Benfica ikiwa nyumbani Ureno iliinyuka Bordeaux ya Ufaransa bao 1-0. Timu hizo zinatarajiwa kurudiana wiki ijayo kujua zipi zitakazopenya robo fainali.

Kagera yametemsha kibarua Charles Kilinda

 
MABAO mawili kila moja katika kipindi imeiwezesha klabu ya Kagera Sugar kuzikamata timu za Simba, Mtibwa Sugar na Coastal Union katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kagera ilipata ushindi huo wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu na kusababisha kocha wa maafande hao, Charles Kilinda kutangaza kuachia ngazi kuinoa timu hiyo.
Kagera ilipata ushindi huo katika mechi iliyochezwa jana kenye uwanja wa Chamazi, ambapo bao la kwanza liliwekwa kimiani na Mnigeria, Darlington Ennyima katika dakika ya 33 bao lililodumu hadi mapumziko.
Bao la lililoihakikishia Kagera pointi tatu na kufanye ikifikishe pointi 31 sawa na klabu tatu zilizotajwa hapo juu, liliwekwa kimiani na Juma Nade katika dakika ya 63.
Hata hivyo Kagera imeishia kushika nafasi ya sita nyuma ya Mtibwa Sugar, kwa vile Mtibwa imefunga mabao 22 moja zaidi yao japo uwiano wa mabao ya kufunga wanalingana.

Simba itakayoshuka dimbani Jumapili inaendelea kubaki nafasi ya tatu ikifuatiwa na watakaoumana nao siku hiyo Coastal Union, japo timu hiuzo zinatofautiana mechi walizocheza mpaka sasa.

Msimamo kamili wa Ligi Kuu baada ya mechi ya jana ni:
                             P  W  D  L  GF GA  GD Pts
1 Yanga               18 13  3   2   35  12   23  42
2 Azam                18 11  3   4   31  15  16   36
3 Simba SC          18  8   7   3   26  15  11   31
4 Coastal U          19  8   7   4   21  16   5    31
5 Mtibwa             20  8    7   5   22  18   4   31
6
Kagera Sugar    20  8    7   5   21  17   4   31
7 Ruvu Shooting  18  8    5   5   21  17   4   29
8 JKT Oljoro       19   6   6   7   20  22  -2   24
9 Mgambo JKT    20  7   3   10  14  19  -5  24
10 TZ Prisons      20   4   8   8   11  17  -6   20
11 JKT Ruvu       19   5   4  10  16  30 -14  19
12 Polisi Moro    18   3   6   9   9   18    -9  15
13 Toto African  19   2   8   9  15  27  -12  14
14 African Lyon  20  3   4  13 13  32  -19  13