STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, June 29, 2013

Golden Bush Veterani wainyuka Chuo Kikuu Veterani 2-1


Beki wa Chuo Kikuu veterani Ernest akimtoka Kudra Omar katika pambano lao la leo

Kudra Omar akichuana na beki wa Chuo Kikuu katika mechi yao ya leo
Beki wa Chuo Kikuu akihamisha mpira langoni mwake huku kipa wake Idd akimshuhudia

Heka heka langoni mwa Chuo Kikuu
Ernest akikokota mpira mbele ya Kudra Omar
Nasafisha! Beki wa Chuo kikuu akihamisha  mpira langoni mwake
Onesmo Wazir 'Ticotico' akionyesha kiwango dimbani

Kiungo Shija Katina (8) wa Chuo Kikuu akimtoka Salum Athuman 'Mbududu' wa Golden Bush
Viungo nyota wa zamani nchini Shija Katina (8) na Salum Athuman wakionyeshana kazi
Hupati kitu hapa 'Mbududu'
Shija Katina akimiliki mpira mbele ya Abuu Ntiro

Benchi la Chuo Kikuu likiwa haliamini kama wamelala nyumbani
Beki wa kushoto wa Chuo Kikuu, Ernest (16) akitafuta mbinu za kumtoka Omar Mgonja wa Golden Bush, huku Yahya Issa naye akimpigia mahesabu
MABAO mawili yaliyotumbukizwa wavuni na nyota wa zamani wa Yanga, Kudra Omar na Abuu Ntiro asubuhi ya leo yalitosha kabisa kuipa ushindi wa mabao 2-1 timu ya Golden Bush Veterani dhidi ya wapinzani wa jadi Chuo Kikuu Veterani katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa Chuo Kikuu.
Golden Bush waliochezesha kikosi tofauti na kile walichokitangaza awali, ilianza kutanguliwa kufungwa bao kupitia kwa Paul mshambuliaji aliyekuwa akiikosesha amani ngome wa Golden Bush iliyokuwa chini ya Salum Swedi 'Kussi', Yahya Issa, Shomari na Omar Mgonja na kipa Aman Simba.
Hata hivyo Golden Bush iliyokuwa ikiongozwa katika safu yake ya ushambuliaji na Kudra Omar, Abuu Ntiro, Onesmo Waziri 'Ticotico' wakiungwanishwa vyema katikati na Godfrey Bonny 'Ndanje' Salum Athuman 'Mbududu'walirudisha bao hilo kupitia kwa Kudra Omar.
Dakika moja kabla ya mapumziko, Golden Bush waliongeza bao la pili lililofungwa na Abuu Ntiro baada ya kutokea pia nikupige klatika lango la Chuo Kikuu lililokuwa chini ya kipa Idd aliyejitahidi kuokoa mabao licha ya kwamba amezoeleka kucheza mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ya wachezaji na kuongeza kasi ya mchezo, na hasa Chuo Kikuu Veterani ambayo ilikuwa ikiunganishwa vyema na Shija Katina aliyeng'ara dimba la kati ambayo ilicharuka kutaka kusawazisha bao lakini kikwazo kikawa ukuta wa wapinzani na hasa kipa Amani.
Mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi aliyelichezesha vyema pambano hilo, Mwenyekiti wa Chuo maarufu kama 'Obama', ilipolia Golden Bush walikuwa wababe mbele ya wapinzani wao waliokuwa uwanja wa nyumbani kwa kuwalaza mabao 2-1.

UFUNGUZI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP DIALOGUE 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa umri wa CPTM 29ers waliohudhuria mkutano wa Smart Partneship Dialogue 2013 wakati wa ufunguzi rasmi wa mkuatno huo unaoshirikisha watu zaidi ya 800 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar es salaam Ijumaa Juni 28, 2013
Rais Kikwete na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Mjadala ukiendelea
Rais wa Sri Lanka akishiriki mjadala na vijana wa CPTM 29ers
Rais Omar Bongo katika mjadala huo
Kijana akichangia
Vijana wakichangia mjadala

Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano katika mjadala

Kijana akichangia katika mjadala
Rais wa Sri Lanka na Dkt Mihaela Smith wakifuatilia mjadala



Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akisalimiana na vijana hao
Wanahabari wa ndani na nje ya nchi wakirekodi tukio hilo la kihistoria
Wageni mbalimbali katika mkutano huo
Ujumbe wa Swaziland
Ujumbe wa Tanzania
Meza kuu
Meza kuu
Vijana nwa THT wakitumbuiza


Viongozi mbalimbali
THT wakitumbuiza
Meza kuu wakifurahia onesho la THT
Wanafunzi wakiimba kwa furaha

Meza kuu wakishangilia
Sehemu ya wageni(picha na Ikulu)

LINA ALLAN NDIYE MISS REDD'S KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI.

 MSHINDI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI LINA ALLAN AKIWA ANAFURAHIA BAADA YA KUWA MSHINDI WA KWANZA
  MSHINDI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI LINA ALLAN AKIWA NA WASHINDI WENGINE AMBAO WALISHINDA TANO BORA
 MSHINDI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI LINA ALLAN AKIVISHWA TAJI LA USHINDI NA MSHINDI AMBAYE ALIKUWA ANASHIKILIA TAJI HILO NAOMI JONES

 
 WASHIRIKI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI WAKIWA WANAONESHA VIPAJI
 BWANA HIDAN ERICCO AKITANGAZA WASHINDI WALIOINGIA KATIKA TANO BORA
 WASHINDI WALIOFANIKIWA KUINGIA KATIKA TANO BORA 

PICHA NA MBEYA YETU