STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 10, 2013

JB Shikamoo Mzee Majuto

King Majuto

WAKATI filamu yake mpya ya Zawadi Yangu ikiendelea kukimbiza sokoni kwa sasa, muigizaji nyota  wa filamu nchini, Jacob Stephen 'JB' yupo mbioni kuachia kazi nyingine iitwayo 'Shikamoo Mzee'.
JB anayefahamika pia kwa jina la 'Bonge la Bwana' alisema filamu hiyo mpya amewashikirikisha  wasanii wakongwe wa fani hiyo kama Chuma Suleiman 'Bi Hindu' na Amri Athuman 'King Majuto'.
Muigizaji huyo ambaye pia ni mtunzi, mwandishi wa miswada, muongozaji na mtayarishaji filamu  alisema kuwa wasanii wengine walioshiriki filamu hiyo itakayoachiwa mwishoni mwa mwezi huu ni  Seleman Abdallah 'Barafu', Shamsa Ford na wakali wengine.
"Baada ya kuwapa mashabiki wangu 'Zawadi Yangu' safari hii wajiandae kupata burudani nyingine  kupitia 'Shikamoo Mzee' ambayo nimeigiza tena na King Majuto, Bi Hindu na wakali wengine,"  alisema.
JB alisema amejiwekea malengo kwamba kila mwaka afyatue filamu moja na mkongwe King  Majuto na kazi hiyo inakuja baada ya makamuzi makubwa waliyofanya kwenye 'Naenda kwa  Wanangu'.
"Kwa walioiona 'Naenda kwa Mwanangu' wanaweza kuelewa maana ya makamuzi, ila safari hii ni  funika bovu kwani mkongwe huyu akishirikiana na Bi Hindu wamefanya majambo yasiyo ya  kawaida wakisapotiwa na mimi mwenyewe JB, Shamsa Ford, Barafu na wengine," alisema JB.

K-Guitar wa Bana Marquiz Usikate Tamaa


K- Guitar
MUIMBAJI wa bendi ya muziki wa dansi, Kelvin Nyoni 'K Guitar', amefyatua wimbo mpya binafsi  uitwao 'Usikate Tamaa' katika miondoko ya Bongofleva akiwa mbioni kutoa albamu yake nje ya  bendi hiyo inayoongozwa na mkongwe, Tshimanga Kalala Assosa 'Mtoto Mzuri'.
Akizungumza na MICHARAZO, muimbaji huyo wa zamani wa bendi ya Victoria, alisema wimbo huo  ambao anajiandaa kuanza kuusambaza katika vituo vya redio ni kati ya nyimbo tatu zilizokamilika  kwa ajili ya albamu yake ijayo.
K-Guitar alisema hata hivyo kwa sasa anasaka meneja wa kumsaidia kusimamia kazi zake, akiamini  bila usimamizi wa mtu makini lengo lake la kutoa albamu halitaweza kufanikiwa kama atakavyo.
"Nimerekodi wimbo mmoja uitwao 'Usikate Tamaa' huku nyingine mbili za 'Subira' na 'Zawadi'  zikiwa zinasubiri kurekodiwa, ila nitafanya hivyo nikifanikiwa kupata meneja wa kusimamia kazi  zangu," alisema muiimbaji huyo ambaye pia ni mahiri kwa kupiga gitaa la rythim.
Muimbaji huyo alisema kwa vile yeye ni mwanamuziki wa Bana Marquiz akipata meneja wa  kumsimamia kazi zake binafsi kama msanii wa kujitegemea itamsaidia kutumikia 'mabwana wawili'  bila tatizo.
Kabla ya kuibukia kwa Assosa, muimbaji huyo aliwahi kuachia wimbo katika muziki wa kizazi kipya  uitwao 'Mapenzi Siyo Pesa' ambao ameurudia akiwa na Bana Marquiz aliyonayo tangu mwaka  2010.

SUPER D KUHAMASISHA NGUMI KATIKA MIKOA 16

SUPER D AKIWA NA VIFAA VYAKE VYA KUFUNDISHIA MASUMBWI

KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' yupo katika ziara ya kutembelea mikoa mbalimbali hapa nchini tangia mwishoni mwa mwezi uliopita ambapo mpaka sasa katika ziara yake hiyo kesha tembelea mikoa kadhaa ya Tanzania Bara akianzia na Tanga,Moshi,,Arusha,Karatu,Babati Mwanza ,Shinyanga na Kahama


Ziara hiyo yenye lengo la kuhamasisha mchezo wa ngumi kwa vijana na kuwapa mbinu mpya baadhi ya makocha wa mikoa husika ili mchezo wa ngumi uweze kusonga mbele ingawa mchezo huo unapendwa na wenga na kukwepwa na wadhamini ndicho kitu kinachokifanya mchezo wa masumbwi uonekane umeshuka hadhi yake wakati bado upo juu

SUPER D akiwa MWANZA

Akizungumzia safari hiyo Super D '' Amesema safari hiyo ni ya manufaa sana kwa watu wa mikoani kwani bado mikoa mingi atatembelea kutoa elimu ya mchezo huo na kuhamasisha vijana wengi wajiunge na mchezo huo kwani yaweza kuwa ni ajira yao 

Super D ambaye ni kocha wa kwanza kutoa mafunzo yake kwa njia ya DVD zilizochanganywa na clips mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo ni chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani wasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

DVD zina mabondia wakari wanaotamba Duniani kama vile Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi 

Super D aliongeza kuwa mikoa mingine atakayotembelea ni Tabora,Singida,Dodoma,Morogoro,Iringa,Mbeya na Songea

ambapo amewaomba baadhi ya makocha,wadau wa mchezo huo wa mikoa husika ambao ajawai kuonana  mikoa iliyotajwa kuwasiliana nae ili wabadilishane ujuzi kwani kuna wengine awana mawasiliano nao waweza kumpigia kwa 0713 406938 ili kupeana ufundi na ujuzi zaidi wa mchezo wa masumbwi ili usonge mbele  zaidi