STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 15, 2013

Ghana, Misri leo hapatoshi zinakutana kwa mara ya 19

Ghana Black Stars
MABINGWA wa zamani wa Afrika na waliowahi kuwa wawakilishi wa bara la Afrika katika Fainali za Kombe la Dunia, Ghana na Misri leo zinatarajiwa kupepetana katika pambano la awali la hatua ya mwisho wa mchujo wa kuwania fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazili mwakani.
Timu hiuzo zinaumana leo kukamilisha mechi tano za mkondo wa kwanza za mchujo wa mwisho kusaka timu tano za Bara la Afrika zitakaliwakilisha katika fainali hizo za dunia.
Mechi nne za awali zilichezwa mwishoni mwa wiki na kushuhudiwa matokeo ya kusisimua, Ivopry Coast ikiitambia Senegal mabao 3-1, Algeria ikizabuliwa mabao 3-2 na Burkina Faso ugenini, huku Nigeria ikiilaza Ethiopia iliyokuwa nyumbani kwao kwa mabao 2-1 na Cameroon ikivimbiwa na Tunisia na kutoka suluhu ya 0-0.
Pambano la Misri na Ghana zinakumbusha fainali za kombe la Afrika za mwaka 2010 ambapo Ghana walilala bao 1-0 kwa Mafarao. Timu hizo zinakutana leo ikiwa ni mara ya 19 katika michezo ya kimataifa ikijumuisha mechi za mshindano na ile ya kirafiki.
Katika mechi 18 za awali baina ya timu hizo Ghana imekuwa wanyonge ikibamizwa mechi 9 na kushinda michezo minne tu na kuambulia sare katika mechi tano.
Hata hivyo mechi hiyo inazikutanisha Ghana wakionekana wazuri zaidi, licha ya Misri nao kutishwa ikiundwa na wachezaji nyota vijana na kufanya iwe vigumu kutabirika atakayemtesa mwenzake kabla ya kurudiana tena mwezi ujao na kuamua hatma ya timu moja wapo katika uwakilishi wa fainali hizo za dunia.

Waislam wakiungana na wenzao ulimwenguni kuswali Eid El Hajj leo

Waumini wa Kiislam wakisikiliza hotuba mbili za Eid el Hajj leo asubuhi
Sheikh akitoa hotuba baada ya sala ya eid leo
Waumini wakiwa katika iktidar wakati wa Swala ua Eid leo
Waumini wakisudu katika swala la Eid iliyoswaliwa viwanja vya Jangwani na maeneo mengine pamoja na misikiti kadhaa inayofuata kalenda ya Kiislam ambapo leo inaoonyesha ni Mwezi 10 Mfungo Tatu
WAUMINI wa kiislam wa nchini Tanzania leo wameungana na waumini wengine wa dini hiyo duniani kuswali swala ya Eid El Hajj kuashiria kumalizika kwa ibada ya Hijja ambapo Mahujaji leo wanachinja wanyama baada ya jana kusimama Arafa.
Karibu dunia nzima wapo katika shamrashamra hizo za Eid tofauti na hapa Tanzania ambapo baadhi wanakusudia kusherehekea kesho kwa mujibu wa Baraza Kuu la Kiislam Tanzania (BAKWATA) waliowatangazia waumini Eid ni kesho Jumatano...! MICHARAZO iunawatakia waumini woite Eid Njema Inshallah.