STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 14, 2014

Huyu ndiye Awadh Juma 'Maniche' aliyewaliza Yanga mara mbili NMJ

Awadh Juma (kushoto) akipambana katika NMJ-2 jana ambapo Simba ilishinda mabao 2-0, moja likifungwa naye
Awadh Juma alivyokuwa akishughulika jana wakati wa pambano la NMJ-2
http://api.ning.com/files/7TcBzbi1eXpJR97d5lfhSWcQtc2ahMajCip36ZbbxLxyrWWQt56ydgr6kDAFSd9mG53EzvsTkDVjWGcWBg7FRE4MWF0UPSdm/KASEJA7.JPG
Awadh Juma alivyomtesha Kaseja katika NMJ-1
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRQqeYRvyVSRUl8NThI45bfeCdna0GQhYraS22s2Mv2wz_j1xTJP7fN1ykK1XpqT4AB_HWD3931ii_3f5SSeyFHMTACxuGpUXbmV-tGmhApgYS9FzJiAM_5FKW82v4BIc3Wfs_giBhRmTT/s1600/DSC00998.JPG
Awadh Juma akiwa na Jonas Mkude
KATIKA pambano la Nani Mtani Jembe lililochezwa mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa, alikuwa mmoja wa wafungaji wa mabo matatu yaliyoizamisha Yanga mbele ya Simba akiwa ndiyo kwanza ametoka kusajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar.Mara baada ya pambano hilo ambalo Yanga walilala mabao 3-1, Awadh Juma maarufu kama 'Maniche' alizungumza na MICHARAZO katika mahojiano maalum na kudai kuwa alijisikia furaha kubwa kucheza mechi yake ya kwanza kubwa inayohusisha watani wa jadi wa soka nchini, Simba na Yanga na kufunga bao.
Maniche alisema lililomsisimua zaidi ni kitendo cha kumzidi ujanja kipa bora nchini na Afrika Mashariki, Juma Kaseja.
Kiungo mshambuliaji huyo alifunga bao la tatu lililo gumzo kwa sasa na lililomletea kizaazaa kipa Kaseja akisakamwa akidaiwa 'aliiuza' Yanga kwa klabu yake ya zamani.
wakati mashabiki wakiamini labda alibahatisha tu kwenye mchezo huo, Maniche kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa ana bahati ya michuano hiyo ya Nani Mtani Jembe baada ya jana kufunga bao la kuongoza la Simba lililoisaidia kupata ushindi wa pili mfululizo dhidi ya Yanga.
Mchezaji huyo alifunga bao la kwanza katika dakika ya 31 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa kizembe na kipa Deogratius Munishi 'Dida' na yeye kuukwamisha kulia mwa lango ya Yanga lililokuwa likimdokolea macho.
Bao hilo lilitokana na mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa kiufundi na Mganda Emmanuel Okwi na kuchangia kummsha hamasa ya vijana wa Msimbazi walioandika bao la pili dakika chache kabla ya mapumziko kupitia kwa Elias Maguli aliyeuwahi mpira wake wa kichwa uliogonga besela na kurudi kwake.
Maniche aliyemtetea Kaseja baada ya kumtungua mwaka jana, alisema amefurahi sana kufunga tena kwenye michuano hiyo na kusaidia Simba kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Alisema kuwa kujiamini na kuwa katika kikosi bora chini ya kocha Patrick Phiri ndiyo siri ya ushindi wa timu yao na sababu ya yeye kuendeleza kuwaliza Yanga.
Mchezaji huyo anadai alichofanya katika mechi hiyo ya Nani Mtani Jembe, ni sehemu tu ya ujuzi alionao katika soka na kuwaahidi wadau wa Simba kusubiri kupata mambo makubwa wakati ngwe Ligi Kuu Tanzania Bara itakapoendelea tena kuanzia Desemba 26.
Kiungo huyo aliyezaliwa miaka 22 visiwani Zanzibar akiwa mtoto wa pili kati ya saba wa familia yao anasema angependa kufanya makubwa katika ligi ili aweze kupata nafasi ya kujitangaza katika soka la kimataifa kupitia Simba.
Nyota huyo wa zamani wa klabu za Jang'ombe, New National, Leba, Tanzania Soccer Academy (TSA) kabla ya kutua Mtibwa Sugar miaka mitatu iliyopita, anasema anatamani kucheza soka la kulipwa Ulaya.
Maniche anayependa kula ndizi kwa nyama na juisi halisi ni shabiki mkubwa wa klabu za Barcelona na Manchester United.
Juu ya pambano analokumbuka kichwani mwake ni lile la Zanzibar Heroes dhidi ya Sudan katika michuano ya Chalenji ya mwaka 2009.
"Naikumbuka mechi hiyo kwa vile ilikuwa ya kwanza kwa michuano ya Kombe la Chalenji," anasema.
Mchezaji huyo anayetaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kurekebisha mfumo wa ligi na kuongeza mashindano mengi ili kuwapa nafasi wachezaji kukuza viwango vyao.
"Kuwepo kwa michuano mingi kama ile ya Super8  itawasaidia wachezaji, pia mfumo wa ligi ubadilishwe kwani unafanya wachezaji wawe mapumziko muda mrefu bila sababu," anasema.
Maniche aliyevutiwa na kiungo nyota wa zamani wa Tanzania, Shekhan Rashid, japo kwa sasa anamzimia kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima, anasema  kubadilishwa mfumo wa soka nchini ni 'muarobaini' wa mafanikio ya Taifa Stars.
Anasema Stars inaangushwa na mambo madogo ambayo yakirekebishwa  huenda ikaifanya timu hiyo ikatamba kama mataifa mengine, huku akiwataka wachezaji wenzake kujituma na kuzingatia nidhamu na miiko ya soka.
Juu ya tukio la furaha Awadh anasema ni kitendo cha kusajiliwa na Simba na anahuzunishwa na tukio la ajabu lililowahi kumpata wakati akiwa uwanja wa Ndege kuelekea Thailand kucheza soka la kulipwa bada ya pasi yake ya kusafiria kushindwa kusoma kwenye mitando na kukwama kuondoka.
"Yaani ni kama miujiza, nilifaulu majaribio yangu ya soka la kulipwa Thailand, nikarejea kusubiri kutumiwa tiketi nikaanze kuitumikia, siku ikawadiwa tiketi ikaja sasa nikiwa uwanja wa ndege amini usiamini pasipoti yangu iligoma kusoma na kukwama safari," anasema.
"Mpaka leo nashindwa kujua ilitokana na nini, ila sijakata tamaa Mungu atanisaidia nitatimiza ndoto za kucheza soka la kulipwa," anaongeza.
Awadh Juma Issa, alianza kucheza soka la chandimu tangu akisoma Shule ya Msingi Jang'ombe na kuendelea wakati akiwa Sekondari ya Mtakuja aliposoma hadi kidato cha pili na kuhamia Makongo baada ya kumvutia Kanali Mstaafu Idd Kipingu kupitia michuano ya shule visiwani Zanzibar.
Kabla ya kuja Makongo alishaanza kung'ara katika soka kupitia Jang'ombe, New National na Leba Fc, na alipokuwa Makongo alichaguliwa TSA kabla ya Mtibwa kumchukua na hivi karibuni kutua Simba.

Droo ya 16 Bora kesho, Arsenal roho juu!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJm6uGPnfQYuZOYeIc6TREJk992xYdYmz-I1iHvSBEMs3xq5IGc3xOP-kQuRWo5qBaC0NBAsixBOpvEcmcMhO-kwjhkK2I3QiWKHcqNck2Wsbas89EOkdxrxStVgX2ThqFHg5pkmFznNXU/s1600/UEFA-Champions-League-Draw-Group-Stages.jpgRATIBA ya Mtoano wa hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kupangwa kesho ambapo itafahamika klabu gani itakutana na nani katika hatua hiyo, huku presha kubwa ikiwa kwa klabu ya Arsenal ambayo ilimaliza nafasi ya pili katika kundi D nyuma ya Borussia Dortmund.
Kwa mujibu wa upangwaji wa hatua hiyo timu zilizoongoza hatua ya makundi zitatangulia kwenye vyungu kisha kutafutwa timu za kucheza nazo miongoni mwa timu nane zilizomaliza nafasi ya pili, huku kukiwa na hatari kwa Arsenal kuangukia tena mikononi mwa kigogo kati ya Real Madrid, Barcelona au Bayern Munich ambao zimekuwa zikimnyima raha kocha Arsene Wenger kiasi cha kulaumu sare ya 3-3 iliyopata kwa Dortmund na kumweka katika karinyekarinye hiyo.
Jumla ya timu 16 zimefaulu hatua hiyo baada ya mie4zi kadhaa ya kuchuana hatua ya awali na makundi, Real Madrid wakiendeleza rekodi ya kushinda mechi zake kwa mwaka wa pili mfululizo kwa asilimia 100 na kuongoza kundi B.
Mabingwa watetezi hao , Atletico Madrid, Fc Barcelona, Monaco, Chelsea, Bayern Munich, Porto na Dortmund ndiyo walioibuka kinara wa makundi yao, wakati timu za  Manchester City, Arsenal , Bayer Liverkursen, Shalke 04, Shakhtar Donetski, PSG, Juventus  na Basel wakimaliza nafasi ya pili.
Timu zilizomaliza kwenye nafasi ya tatu zenyewe zimeangukia kwenye michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya ambayo pia droo yake inatarajiwa kupangwa kesho.
Timu zilizoangukia huko kutoka Ligi ya Mabingwa ni pamoja na Olympiakos Pirates, Liverpool, Zenit Petersburg, AS Roma, Anderlecht, Ajax Amsterdam, Sporting Lisbon na Athletic Bilbao.
Unadhani unaweza kutabiri nani na nani watakaokutana katika hatua hiyo ya 16 Bora ya Mabingwa Ulaya kabla ya kuja kushuhudia Fainali baadaye Juni 6, 2015?

HATARI! Watu 6 wafa kwa kuchinjwa kama Kuku Bukoba

Kanisani alipouawa mwalimu Ng"wandu
KWA kipindi cha miezi miwili tu, kuanzia Octoba 9 hadi Desemba 4 mwaka huu, ambapo jumla ya vijana  6 wameuawa katika mazingira ya kutatanisha,  watatu wamechinjwa katika kata ya Kitendaguro, 1 katika kata ya Rwamishenye, huku wawili wakichinjwa katika kata ya Kibeta ndani ya manispaa, huku wananchi wakishangaa ukimya wa mamlaka bila kuchukua hatua.

Tarehe 09 Oktoba, aliyeuawa mwalimu DIONIZ NGW’ANDU wa shule ya sekondari Kagemu, alipokuwa katika kanisa la PAGT, baada ya kukatwa kichwa na kitu chenye ncha kali, huku jamaa yake aliyekuwa mlinzi katika kanisa hilo siku hiyo akijulikana kwa jina mojala THEMISTOCRES akisalia na ulemavu wa maisha, kama alivyoeleza  mchungaji wa kanisa hilo FAUSTINE JOSEPH. 

Siku kati ya 5 au saba badaye, mwili wa kijana ambaye hakutambuliwa majina wala sura, ulikutwa umeharibiwa kwa kunyofolewa macho, huku ukitupwa kando mwa shamba la mmoja wa wakazi wa Kitendaguro, ambapo Anakret Laurent Kyaishozi miaka 30 alikuwa shuuda, aliueleza mtandao huu kuwa mwilihuoulichukuliwa na polisi mpaka sasa hawajajua ninikiliendelea.

Kando na hayo, familia ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka 37 Erick Kashaga akiacha mjane Sofia Mozes miaka 32 na watoto saba, imesalia katika mvutano mkubwa,na familia ya bwana Levocatus , ambaye mpaka sasa yuko mikononi mwa jeshi la polisi, huku jamaa zake wakielezwa kuwa uchunguzi unaendelea.
Kaburi la Mozes Kashaga
 Levocatusi ni kijana  mwenye umri wa miaka 33 huku akiwa na watoto watatu wawili wakizaliwa na mke wake wa Katoma walieachana, na mmoja akizaliwa na mke anayeishi naye Kitendaguro, Bi Ajat au Betrida mwenye umri wa miaka 32, alikamatwa baada ya kutajwa kuwa alitambuliwa na kijana aliyekuwa na marehemu wakatiwa tukio .
Mzee Rumumba akionesha eneo alipochinjwa Mozes
Mzee SILIDION RUMUMBA mwenye umri wa miaka 73,  ndiye mmiliki wa kilabu cha pombe, ambacho dakika za mwisho marehemu aliondoka hapo muda wa saa tano usiku, akiwa na jamaa zake wawili.

Ndani ya dk kama mbili baadaye, liyetajwa kwa jina moja tu la Eriki alirudi nyumbani kwa mzee SILIDION RUMUMBA akiwaeleza kuwa wamevamiwa na mtu ambaye alimtaja jina, huku akisema kuwa hana hakika kama watamkuta hai Kashaga, ilhali akitoa taarifa hizo kimyakimya, pasi na kupiga kelele wakati wa tukio,jambo ambalo linawashangaza wengi, kwasababu marehemu ameuawa karibu kabisa na makaazi ya watu.
Mama mzazi wa Mozes
Kando na maelezo hayo, nimetaka kusikiliza ushuuda wa Erick aliyethibitisha kuwa alishuudia mauaji hayo, lakini nyumbani kwaojamaa zakewalisema kuwa huwezi kumwona sababau wamemficha sehemu baada ya kutishiwa na mkewa mtuhumiwa.

Hayo yamesalia katika familia hizo ndani ya kata ya Kitendaguro, huku katika kata ya kibeta, lawama kubwa zikiangushwa kwa mamlaka, kuwa hawajaonesha juhudi zozote  baada ya kuuawa kijana GOODRUCK FRANCIS aliyekuwa na umri wa miaka 38, ambapo  taarifa za awali zinaonesha kuwa aliuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana, ikiwa ni kando kando mwa barabara ya mtaa wa Kibeta Amjuju.
Bi Stella Lenatus amesema amekata tama kwasababu tangu ahojiwe, ameenda kituoni kujua taarifa za mdodgo wake na kuambiwa asubiri walikuwa bize na kazi nyingine muhimu.
Hapo kustoto pichani ndipo aliuawa Gudrack eneo la Kibeta Anyama.
Sambamba na wanaouawa pasipo kutambulika majina na makwao ndani ya manispaa ya Bukoba, Ernest Kato ni kijana aliyeuawa mwezi novemba akiwa na miaka32,katika mtaa wa Bugezi kata Rwamishenye, majira ya usiku, na kutambulika asubuhi ya tarehe iliofuata kwa kukutwa amechinjwa, huku akiacha mjane na mtoto mmoja, ambaye hatahivyo  amekimbia kwa kuhofia naye kuawa.

Mmoja kati ya wanafamilia wa marehemu Ernest, ameomba jina lake lihifadhiwe, pamoja na kusema kuwa wanaishi kwa hofu kubwa kiasi cha kujipangia muda wa kurudi nyumbani mapema nyakati za usiku, na shughuli zimesimama.

Mauaji ya  mwisho hadi ninakamilisha makala haya, ni alivyouawa Joran Rutulaniisa, mkaazi wa Kibeta magoti, nilifika eneo la tukio muda mfupi tu baada ya polisi kuubeba mwili wake lakini taarifa za ndugu ambao hatahivyo wanahofu ya maisha yao, ni kuwa nduguyao  ameuawa kwa aina ile ile ya vifo vya kukatwa koromeo.
Marehemu Rutu enzi za uhai wake
Tetesi ambazo bado sijazithibisha, wananchi wanaofanya biashara ya senene, wamelazimika kuanza kujifunga vitu vigumu na tauro shingoni, kama taadhali watakapovamiwa.
Shangazi na mama mdogo wa marehemu kwenye kaburi la Rutu

Baba wa marehemu Rutulanisa
Mauaji nikitendo kisichokubalika kwa mwenyezi Mungu, jambo linalompa shekh mkuu wa mkoa wa Kagera Aruna Kichwabuta,kukemea hali hiyo katika mamlaka na wananchi.
Shekh mkuu wa mkoa, Haruna KICHWABUTA
Makala maalumu sehemu ya kwanza kuhusu mauaji hayo inaruka marudio leo saa moja jioni kupitia 88.5 Kasibante fm Bukoba.

 
Na Mwanaharakati

Hivi ndivyo Simba ilivyoinyoa Yanga mabao 2-0 Nani Mtani Jembe

 Kocha wa Simba, Patrick Phiri akisalimiana na kocha wa Yanga, Marcio Maximo kabla ya mchezo.
Katika pambano hilo lililokuwa kali na la kusisimua, Simba ilipata mabao yake katika kipindi cha kwanza kupitia Awadh Juma 'Maniche' na Elias 'Magoli' Maguli na kuifanya Yanga inyong'onyee kwa mwaka wa pili mbele ya Mnyama baada ya mwaka jana kucharazwa mabao 3-1 katika mchezo kama huo.
 (Picha zote: Francis Dande)
 Emmanuel Okwi akiomba dua wakati akiingia uwanjani.
 Mgeni rasmi Mh waziri wa michezo Dr Fenella Mukangala akisalimiana na wachezaji wa Yanga.
 Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji waSimba.
Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Simba.
Kocha wa Yanga akitafakari.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiwa amenyanyua juu
Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe msimu wa pili uliofanyika leo kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 2-0. 
 Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Mchezo, Dk. Fenella Mukangala akimkabidhi nahodha wa Simba, Emmanuel Okwi Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe.
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Umati wa mashabiki wa Yanga.
 Umati wa mashabiki wa Simba.
Mashabiki wa Simba wakiwa wamebeba mfano wa jeneza kuwakejeli watani zao.
 Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’
 Beki wa Yanga, Kelvin Yondan akimiliki mpira.
 Mwamuzi wa mchezi akimuonyesha kadi ya njano mshambuliaji wa Simba, Simo Serunkuma.
 Kpah Sherman akiokoa moja ya hatari langoni mwake huku Elius Maguri akimzonga.
 Mshambuliaji wa Simba Elius Maguri akichuana na beki wa Yanga, Nadir Haroub.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao la kwanza.
 Hassan Isihaka (kushoto) ana Ramadhani Singano ‘messi’ wakishangilia bao la kwanza la timu yao.
Beki wa Yanga, Oscar Joshua akimtoka Elius Maguri wa Simba.
Shabiki wa Yanga akipata msaada baada ya kuzimia jukwaani.
 Mashabiki wa Simba wakiwa na bango lenye idadi ya mabao waliyowahi kufungwa Yanga.
Leo ni 2-0…..
Burudani zikitolewa uwanjani.
 Mashabiki wakitolewa uwanjani baada ya kuzimia.
 Hali ilikuwa ngumu kwa mashabiki mpaka baadhi yao kuzimia.
Huduma ya kwanza kwa waliozimia ikitolewa.
 Beki wa Yanga, Kpah Sherman akichuana na beki wa Simba, Hassan Isihaka.
 Danny Mrwanda akiwa ameshika kichwa baada ya kukosa bao la wazi.
Ivo Mapunda akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Simon Msuva akichuana na Issa Rashid.
Ivo Mapunda (katikati) akishangilia ushindi na wenzake.
Wachezaji wa Yanga wakiwa na huzuni baada ya kumalizika kwa mchezo.
Yanga wakiwa vichwa chini.
 Medali za washindi.