STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 14, 2014

Droo ya 16 Bora kesho, Arsenal roho juu!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJm6uGPnfQYuZOYeIc6TREJk992xYdYmz-I1iHvSBEMs3xq5IGc3xOP-kQuRWo5qBaC0NBAsixBOpvEcmcMhO-kwjhkK2I3QiWKHcqNck2Wsbas89EOkdxrxStVgX2ThqFHg5pkmFznNXU/s1600/UEFA-Champions-League-Draw-Group-Stages.jpgRATIBA ya Mtoano wa hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kupangwa kesho ambapo itafahamika klabu gani itakutana na nani katika hatua hiyo, huku presha kubwa ikiwa kwa klabu ya Arsenal ambayo ilimaliza nafasi ya pili katika kundi D nyuma ya Borussia Dortmund.
Kwa mujibu wa upangwaji wa hatua hiyo timu zilizoongoza hatua ya makundi zitatangulia kwenye vyungu kisha kutafutwa timu za kucheza nazo miongoni mwa timu nane zilizomaliza nafasi ya pili, huku kukiwa na hatari kwa Arsenal kuangukia tena mikononi mwa kigogo kati ya Real Madrid, Barcelona au Bayern Munich ambao zimekuwa zikimnyima raha kocha Arsene Wenger kiasi cha kulaumu sare ya 3-3 iliyopata kwa Dortmund na kumweka katika karinyekarinye hiyo.
Jumla ya timu 16 zimefaulu hatua hiyo baada ya mie4zi kadhaa ya kuchuana hatua ya awali na makundi, Real Madrid wakiendeleza rekodi ya kushinda mechi zake kwa mwaka wa pili mfululizo kwa asilimia 100 na kuongoza kundi B.
Mabingwa watetezi hao , Atletico Madrid, Fc Barcelona, Monaco, Chelsea, Bayern Munich, Porto na Dortmund ndiyo walioibuka kinara wa makundi yao, wakati timu za  Manchester City, Arsenal , Bayer Liverkursen, Shalke 04, Shakhtar Donetski, PSG, Juventus  na Basel wakimaliza nafasi ya pili.
Timu zilizomaliza kwenye nafasi ya tatu zenyewe zimeangukia kwenye michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya ambayo pia droo yake inatarajiwa kupangwa kesho.
Timu zilizoangukia huko kutoka Ligi ya Mabingwa ni pamoja na Olympiakos Pirates, Liverpool, Zenit Petersburg, AS Roma, Anderlecht, Ajax Amsterdam, Sporting Lisbon na Athletic Bilbao.
Unadhani unaweza kutabiri nani na nani watakaokutana katika hatua hiyo ya 16 Bora ya Mabingwa Ulaya kabla ya kuja kushuhudia Fainali baadaye Juni 6, 2015?

1 comment:

  1. Una blog? Unataka tuweke matangazo kwenye blog yako ulipwe vizuri na utajirike? Basi bonyeza jina langu kisha soma zaidi

    ReplyDelete