STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 14, 2014

SHIME WATANZANIA TUKAPIGE KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

http://4.bp.blogspot.com/-ihy-SS2WtGw/UeLe6kO-DSI/AAAAAAAAvcQ/BSjwoNN55d4/s1600/IMG_0257.JPG
Shime watanzania changamkieni uchaguzi kama hivi, msije mkajilaumu baadaye weatakapochaguliwa viongozi wasiofaa katika eneo lako.
LEO Desemba 14 ni Siku ya Kupiga Kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji, Tarafa na Vijiji.
Shime watanzania hii ni siku muhimu na ambayo yeyote hapaswi kuipoteza.
Hivyo yeyote ambaye amejiandikisha katika orodha ya wapiga kura katika maeneo yao ni wajibu wao kutumia haki yao kwa kwenda kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka kutokana na wasifu wao.
Kitu cha muhimu mzingatie sifa na uwezo wa mtu badala ya kuangalia chama, jinsia, imani ya kidini, kabila au jambo lolote lisilo la tija kwa maendeleo ya eneo husika.
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa tangu kuanzia saa 2 asubuhi mpaka jioni, hivyo yeyote anayetambua wajibu wake kwa maendeleo ya eneo lake na Taifa kwa ujumla aitumie nafasi hiyo adhimu kwa kwenda KUPIGA KURA kuchagua VIONGOZI wanaofaa.
MICHARAZO inawatakia kila la HERI katika zoezi hilo na MUNGU awaongoze kuwachagua WANAOSTAHILI.

No comments:

Post a Comment